Image
Image

Vodacom yaongeza mtandao wa maduka yake ili kusogeza huduma kwa wananchi




Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania,Upendo Richard akishirikiana na meneja wa duka jipya la Vodacom lilillopo eneo la Kimara Stop over jijini Dar es Salaam, Eunice Lulinga (kushoto) kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka hilo,akishuhudia Katikati ni meneja Uhusiano wa nje wa kampuni hiyo Salum MwalimIkikadiriwa kuwa na wateja zaidi ya milioni kumi na moja, kampuni ya simu ya Vodacom imesema itaendelea kuchukua juhudi za makusudi kuweka huduma zake karibu na wananchi ili kuendana na kasi ya ongezeko la wateja sanjari na kupanuka kwa miji.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Mauzo anaeshughulikia usimamizi wa maduka ya Vodacom Upendo Richard wakati wa hafla ya ufunguzi wa duka jipya la Vodacom lilipo eneo la Kimara Stop Over nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Upendo amesema kuwa Vodacom imeendelea kushuhudia ongezeko la kasi la wateja ambao wamekuwa wakiishi maeneo mbalimbali wengi wao nje ya miji hatua ambayo amesema inaipa kampuni yake changamoto ya kuhakikisha huduma zake zinapatikana karibu zaidi bila kuathiri ubora.

"Tunafuraha kubwa leo hii kuzindua duka la 69 kwa nchi nzima likiwa ni la 19 kwa mkoa wa Dar es salaam, Jambo zuri kwa duka hili ni kwamba lipo nje ya mji na hivyo kuwahakikishia wateja wetu kupata kila wanachokihitaji karibbu na makazi yao na maeneo ya shughuli zao za kila siku."

"Miji yetu nayo inapanuka na hatuwezi kuwafanya wateja wetu kuendelea kutegemea maduka yaliyopoameneo ya katikati ya mji ama karibu na mijini lazima tuwafikishie huduma mahali walipo hata kama ni nje ya miji ili kuwpaunguzia gharama ya muda na fedha kwa kusafirei kufuata huduma hizo umbali mrefu."Aliongeza Upendo Upendo amewataka wakazi wa Kimara na maeneo ya jirani kulitumia duka hilo ili waweze kuendana na shabaha ya Vodacom ya kuwapunguzia wateja wake gharama huku akiwahakikishia wateja kuwa ubora wa huduama za Vodacom kwenye duka hilo unakidhi vigezo vya ubora wa maduka mengine.

"Tunaleta huduma karibu na wananchi ili kuwapunguzia gharama na kero za kusafiri umbali mrefu nataka niwahakikishe wateja wetu kwamba ubora wa huduma kwenye duka hili ni sawa na za kwenye maduka yetu mengine kama la Oysterbay, Mlinai City na Samora hivyo kwani linapokuja sula la kumhudumia mteja kwetu sisi hakuna tofauti."Alisisitiza Kwa upande wake Meneja wa duka hilo Eunice Lulinga amesema duka hilo litakuwa likitoa huduma zote za Vodacom ikiwemo usjili wa nambari, Swim Swap, M-pesa.

"Tunawakaribisha wakazi wa Kimara kulitumia duka hili kwa mahitaji yao ya Vodacom, tunatambua umuhimu wa huduma bora na kuweka tabasamu kwenye uso wa mteja wetu muda wote ambao Vodacom inawahudumia wateja wake."Alisema Eunice. Akizungumzia umuhimu wa duka hilo kwa wateja, Mkazi wa eneo la Kimara Stop Over ambae pia ni mteja wa Vodacom Mohamed Salim amesema ni ukombozi mkubwa kwao kwa kuwa awali walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hasa kwenye duka la Mlimani City.

"Nikiwa mteja wa Vodacom najisikia furaha kubwa kuona Vodacom imetujali na kutuletea huduma karibu yetu, tunalipokoea kwa furaha sana kutokana na ukweli kwamba litatupunguzia gharama amabzo tulikuwa tukilamika kuingia kwenda hadi Mlimani City."Alisema Salim Salim amesema anatambua kuwa eneo la Kimara kama yalivyo maeneo mengine ya nchi yana uhitaji mkubwa wa huduma za Vodacom hasa M-pesa, usajili na huduma za kupatiwa laini mpya ya simu kutokana na sabbau mbalimbali ikiwemo kupoteza.

Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuongeza mtandao wa maduka yake hatua ambayo imekuwa ikipongezwa na wananchi na wadau wengine hasa kutokana na jinsi jamii inavyoitegemea M-pesa katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiibiashara.

CHANZO WAVUTI.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment