Image
Image

HII NDIO TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI.



[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


“PRESS RELEASE” TAREHE 23. 10. 2013.

WILAYA YA MBARALI –  AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.

MNAMO TAREHE 22.10.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKOMBWE, KATA YA  UBARUKU, TARAFA YA  RUJEWA,  WILAYA YA MBARALI  MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI T.656 BDG AINA YA LIFAN IKIENDESHWA NA WAKATI S/O CHARLES, MIAKA 22, MBUNGU, MKAZI WA MKOMBWE,  LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO AGREY S/O MPWEPWA, MIAKA 5, MSANGU, MKAZI WA KIJIJI CHA MKOMBWE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA  MISHENI RUJEWA AMBAYE  MWILI WAKE UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. AIDHA KATIKA AJALI HIYO MWENDESHA PIKIPIKI ALIJERUHIWA NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.



WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUGONGA GARI NYINGINE KWA NYUMA NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.

MNAMO TAREHE 22.10.2013 SAA 19:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MACHIMBO, KATA YA UJELELE, TARAFA YA  RUJEWA,  BARABARA YA  MBEYA/IRINGA   WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI  T.964 AUN/T.730 BPL AINA YA  SCANIA TANKI LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMORA S/O PETER, MIAKA 35, MHEHE, MKAZI WA DSM,   LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.641 AQQ/ T.935 AUV AINA YA  SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALLY S/O SALIM, MIAKA 38, MPARE MKAZI WA DSM NA KUSABABISHA KIFO UTINGO WA GARI T.964 AUN/T.730 BPL ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA  HAMAD S/O ? NA MAJERUHI KWA DEREVA SAMORA S/O PETER AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA  MISHENI CHIMALA, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI  T.964 AUN/T.730 BPL. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA  MISHENI CHIMALA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA  CHUNYA  – KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI

MNAMO TAREHE 22.10.2013 MAJIRA YA  SAA 05:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA  MAFYEKO , TARAFA YAKIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO  WALIMKAMATA KILINGO S/O FURAHISHA, MIAKA 36, MKIMBU, MKULIMA, MKAZI WA BITIMANYANGA  AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI KILO KUMI [10] ZA NYAMA YA TWIGA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI NYARA ZA SERIKALI ISIVYO HALALI  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU/KIKUNDI KINACHOFANYA SHUGHULI ZA UWINDAJI HARAMU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment