Image
Image

IGP MWEMA AUNDA TIMU MAALUMU YA KUPAMBANA NA MAJANGILI.



SIKU moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki kumtuhumu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha (RCO), Dawal Nyenda, kusaidia majangili kutoroka nje ya nchi, jeshi la polisi limech
ukua hatua ya kuunda timu kuchunguza tukio hilo.

Wakati hayo yakijiri, RCO Nyenda amesema yote yanayotokea anamuachia Mungu, na kwamba hawezi kusema chochote kwa sababu anamheshimu Kagasheki kama mkuu wake wa kazi.

Akizungumza na NIPASHE Jumapili, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Advera Senso, alisema Mkuu wa jeshi hilo nchini, (IGP) Said Mwema, ameteua timu maalum ya watu watakaokwenda jijini Arusha kuchunguza ili kupata ukweli.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo, walipata mshtuko kitu ambacho kilimfanya IGP Mwema kuchukua hatua hiyo na kuahidi matokeo ya uchunguzi huo yatawekwa wazi ili kila mwananchi afahamu.

"Jeshi la polisi linafanya kazi kwa sheria na utaratibu, inapotokea mtumishi hasa kiongozi wa juu kutuhumiwa, hatua mbalimbali zinachukuliwa ikiwamo kufanya uchunguzi kwa mujibu wa sheria," alisema Senso.

Hata hivyo, Senso hakuwa tayari kutaja timu hiyo ina watu wangapi na itachukua muda gani kukamilisha kazi, badala yake alisema wananchi wanatakiwa kuliamini jeshi lao na majibu yatapatikana haraka.

"Unajua kazi za jeshi ni vigumu kukupa taarifa za kila kitu kinachofanyika, kitu muhimu hapa ni kwamba polisi imeshtushwa na jambo hili na kazi hiyo itafanyika kwa uwazi mkubwa," aliongeza kusema.

Alisema timu hiyo itafanya kazi ya msingi ya kusikiliza kila upande na endapo ikibainika kuna ukweli, taratibu za kijeshi zitachukuliwa.

RCO 'NAMUACHIA MUNGU'
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mkoani Arusha, RCO Nyenda alisema mpaka sasa hajui kosa lake, hivyo yote anamuachia Mungu ndiye anayejua ukweli wa jambo hilo.

Alisema yeye hajui chochote juu ya tuhuma hizo kwani waziri hakumlalamikia wala kumtaarifu kama kuna jambo limemkera yeye amelifanya.

"Mimi sijui chochote, taarifa zote nimezisoma kwenye magazeti na kusikia kupitia runinga, muulizeni Kamanda wa Mkoa kama yeye aliambiwa jambo hilo," alisema Nyenda.

Hata hivyo, alisema hawezi kujibizana na kiongozi huyo kwa sababu anamheshimu kama mkuu wake wa kazi.

WAZIRI NCHIMBI: "NIPO NJE"
Alipotafutwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kuzungumzia sakata hilo, alisema kupitia simu yake ya mkononi kwamba hana taarifa kwa sababu yupo nje ya nchi kikazi.

"Ndugu mwandishi habari hii kwangu ni mpya, nakuomba wasiliana na mtu niliyemuachia ofisi kwani kwa sasa nipo nje ya nchi," alisema.

Juzi wakati akitangaza uwapo wa `operesheni tokomeza majangili' nchini kote, Waziri Kagasheki alimtuhumu RCO huyo wa Arusha kushiriki katika mchakato wa kuwatorosha raia wawili wa Saud Arabia ambao walituhumiwa kwa ujangili.

Alisema, watu walikamatwa wakiwa na silaha na baadhi ya vithibitisho vinavyoonyesha walikuwa wakifanya kazi hiyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPIL




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment