Image
Image

WANAMUZIKI WA TANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO MAPEMAAA.

Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Kotilasuti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay.


Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku wajumbe wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia. 


Mwanamuziki Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.
.....................................................................................................................................................................


Na. Mwandishi Wetu. 

Wanamuziki nchini Tanzania wametakiwa kuchangamkia mapema fursa zilizopo kwa kujitangaza na hatimaye  kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya Barcode. 

Kauli hiyo imetolewa na mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania  Profesa Jay wakati alipokuwa akikabidhiwa Barcode kwa ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The Best of Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo zime heat tangu kuanza kwake. 

“nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka kufanya vitu kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie watu wengi zaidi” alisema Jay.

Katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa Tanznia kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ili soko la muziki liweze kutanuka zaidi  kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine wa ndani na nje ya nchi.

Mmari alisema kutumia fursa hizo kwa  wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni makubwa duniani kama CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya kwenye mtandao kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.

Hata hivyo Mmari aliongeza kwa kusema kuwa wanamuziki wa Tanzania hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. 

Kwa upande wake Afisa muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao haziko kwenye mfumo rasmi,

 “ukiangalia mwanamuziki kama Lady Jay Dee mathalani ana wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kama atatangaza na kuuza kazi zake kwenye mitandao hiyo ni wazi atawafikia Mashabiki wake kirahisi zaidi” 

Takwimu za Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji na mauzo ya kazi za mwanamuziki ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama Diamond ambaye kwa sasa ana mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona kupata takwimu sahihi za usambazaji wake.

Pia amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo wanawaumiza sana wanamuziki wa Tanzania  na kuwa  hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. 

Aidha GS1 Tanzania ndio watoaji pekee wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania, na  ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza kwenye Supermarket na masoko ya mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za mistari yaani Barcode.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment