Image
Image

WATU 18 WANUSURIKA KIFO HUKO TUNDAUWA PEWMBA.


WATU 18, wamenusurika kufa akiwemo Sheha wa shehia ya Kilindi Abou Abrahman Salum (67) huku majeruhi Tisa (9) wakilazwa hospitalini,  baada ya gari waliyokuwa wamepanda kuanguka huko katika barabara ya Tundauwa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Tukio hilo lililotokea majira ya saa moja na robo (1:15) za asubuhi ya leo, wakati gari hiyo iliyokuwa ikitokea Tundauwa kwelekea mjini Chake Chake, iliposhindwa kupanda kilima cha Kunguni na kurudi nyuma na kuanguka.
Majeruhi waliopokelewa katika hospitali ya Chake Chake, ambao wamenusurika kifo ni pamoja na Salum Mohamed Salum (70), Haji Salum Mohamed (23), Mzee Juma Saburi (50), Siti Massoud Dadi (60), Saidi Seif Nassor (23).

Wengine ni Ameir Khatib (19), Suleiman Ramadhan Aboud (23), Mariyam Khamis (32), Abdalla Suleiman Abrahman (30), Zubeda Faki (38), Fatma Abeid Khamis (36), Amina Mohamed Abeid (40) na Abou Abrahman Salum (67), wote ni wakaazi wa Kilindi.

Majeruhi wengine ni Fatma Ali Juma (70), Fatma Khamis Ali wakaazi wa shengejuu, Nassor Abdalla Nassor (50) mkaazi wa Kungeni na Rajab Ali Juma (43) mkaazi wa Tundauwa.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Saleh Mohamed Saleh alisema kuwa, gari hiyo iyopata ajali ilikuwa ikiendeshwa na dereva Ali Salum Suleiman (25) mkaazi wa Tundauwa.

Kamanda Saleh aliitaja gari hiyo yenye No Z884 BE yenyeruti Kilindi Chake, ilishindwa kupanda kilima cha Kunguni na kurudi nyuma na kupinduka, huku dereva akishikiliwa na polisi.

Aidha alisema kuwa, katika majeruhi hao Tisa mmoja kati yao  Mzee Juma Saburi, amepelekwa Hospitali ya Mkoani kwa matibabu zaidi baada ya kuumia mguu.

“Ajali imetokea kweli, bahati nzuri hakuna mtu aliyepoteza maisha, ila majeruhi walichunika chunika kidogo katika sehemu za kichwani, mikononi na kutibiwa na kuruhusiwa kwenda zao majumbani”alisema kamanda Saleh.

Hata hivyo aliwataka madereva kuwa na tahadhari sana wakati wanapoendesha gari zao, kwa kuziangalia kabla ya kuanza safari, ili kuweza kuepuka ajili zisizokuwa za lazima.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment