Image
Image

JACK WOLPER AZISALITI FEDHA ZA DALASI,AAMUA KUOKOKA UPYA


 STAA anayefanya vyema katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameamua kurudi katika imani yake ya awali ya Kikristo ikiwa ni miezi michache tangu alipotangaza kubadili dini na kuwa Muislamu.


Novemba 3, mwaka huu (Jumapili iliyopita) paparazi wetu alimnasa Wolper katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama jijini Dar, akisali sambamba na waumini wa kanisa hilo.
Bila ya kificho, Wolper ambaye alipokuwa Muislamu alikuwa akitumia jina la Ilham alisimama na kujitambulisha kama muumini mpya wakati mchungaji wa kanisa hilo alipowataka waumini wapya kufanya hivyo.
Wakati ibada hiyo ikiendelea, Wolper alionekana kuimba pambio kwa hisia kali na ibada ilipoisha, alitoka kanisani huku mkononi mwake akiwa ameshika Biblia.

Paparazi wetu alimfuata Wolper na kumuuliza kilichomfanya arudi kwenye dini yake ya awali, naye alisema kwamba amefanya hivyo kutokana na msukumo wa wazazi wake ambao kwa muda mrefu walikuwa wakipinga kitendo chake cha kuwa Muislamu. 

“Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena, niite Jacqueline kama zamani,” alisema Wolper.
Mwaka jana, Wolper alibadili dini na kuwa Muislamu kutokana na kuwa na uhusiano na Abdallah Mtoro ‘Dallas’. Dallas akiwa nje ya nchi akamtaka Wolper kubadili dini ili akirudi wafunge ndoa ya Kiislamu, Wolper alikubali naacqueline Wolper (kulia), akiingia kanisani na rafiki yake kipenzi

kufanya hivyo katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na kuchagua jina la Ilham. Dallas alirudi nchini lakini wawili hao hawakufunga ndoa bali penzi lao likaingia doa na kumwagana, Wolper akaendelea na msimamo wa imani yake hiyo mpya na mara kwa mara alikuwa akidai kwamba hataiacha dini hiyo pamoja na kumwagana na Dallas


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment