Image
Image

Bingwa wa zamani wa marathoni wa Afrika awataka wanariadha wa Tanzania kumuenzi Theresia Dismas



Bingwa wa zamani wa Afrika wa marathoni, Juma Ikangaa amewataka wanariadha wa Tanzania kumuenzi Theresia Dismas ambaye alikuwa Mtanzania wa kwanza kunyakua medali katika Michezo ya Afrika.
Theresia alitwaa medali ya fedha ya kurusha mkuki katika fainali za Afrika ambazo Tanzania ilishiriki kwa mara ya kwanza 1965 nchini Congo Brazzaville. 
Tayari Serikali imeeleza kuwa Tanzania itashiriki kwenye michezo tisa wakati wa Michezo ya Afrika ya mwakani nchini Congo Brazaville. 
Michezo hiyo ni riadha, ngumi, judo, paralimpiki, taekwondo, kunyanyua vitu vizito, baiskeli, mpira wa meza na kuogelea. Ikangaa alisema michezo ya Afrika ya mwakani inapaswa kutumika kama sehemu ya kumuenzi Theresia. 
Alisema kwa sasa Theresia yupo Kenya, lakini hakuna anayemkumbuka na kumtaja japokuwa ndiye shujaa wa kwanza kuipatia nchi hiyo medali ya michezo ya kimataifa. Aidha nyota huyo aliyeng'ara katika riadha miaka ya 80, alisema, Serikali inapaswa kutenga bajeti ya kutosha katika kufanikisha ushiriki wa Tanzania kwenye michezo hiyo sambamba na timu kuanza maandalizi mapema.

 

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment