Image
Image

Hali ya bondia mashuhuri Muhammad Ali yaimarika.


                                                    Muhammad Ali
Hali ya bondia mashuhuri Muhammad Ali imeimarika vizuri tangu apelekwe hospitali kutokana na ugonjwa wa nimonia. 
Bob Gunnell amesema daktari wa Ali anategemea kumruhusu hivi karibuni. Pia amesema familia ya Ali inaomba ipatiwe faragha na kushukuru kwa maombi yote ya kumtakia Ali apone na awe na afya njema. 
Bondia huyo wa zamani mwenye miaka 72 ambaye ni bingwa mara tatu wa uzito wa juu, mwenye ugonjwa wa Parkinson, alipelekwa hospitali siku ya Jumamosi. Bwana Gunnel hakutoa taarifa zaidi. 
Ali aligundulika kuwa na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984, miaka mitatu baada ya kustaafu ndondi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment