Image
Image

Idara ya Uhamiaji nchini yasema inakabiliwa na tatizo la utoaji hati za kusafiria na tatizo la wahamiaji haramu



Idara ya  Uhamiaji  nchini  imesema  asilimia kubwa ya matatizo yanayoikabili  ni pamoja na  mchakato  wa utoaji  wa hati  za  kusafiria   na tatizo la  wahamiaji  haramu ,yanatokana  na uelewa  mdogo wa  wananchi  juu  ya  majukumu  ya  idara  hiyo na ugumu  unaojitokeza  katika  utekelezaji.

 Akizungumza  katika  mkutano wa  mwaka wa kikao  cha Baraza la Wafanyakazi  wa  idara  hiyo unaofanyika  Jijini   Arusha , Kaimu Kamishna  Mkuu   wa  Idara   ya Uhamiaji, Bw ana    Peniel  Mgonja  amesema,kwa asilimia  kubwa , matatizo hayo  yanatokana na   utamaduni  wa  wananchi  wengi , kutaka  kupata  huduma  kwa  njia  za  mkato  na pia kutumia  muda  mwingi  kulalamikia  mambo  ambayo   utatuzi  wake  uko  ndani  ya  uwezo  wao.

Kuhusu  tatizo  la wahamiaji  haramu,  Bwana Mgonja  amesema  pamoja  na  kuchangiwa  na kuwepo kwa njia nyingi  za  panya  katika  mpaka  wa  Tanzania  na  majirani  zake , pia  linachangiwa na baadhi   ya   wananchi kurubuniwa na  kujikuta  wakiwasaidia  wahalifu.

Akifungua  mkutano  huo , Katibu  Mkuu  Wizara  ya   Mambo ya  Ndani   ya Nchi,   Bwana   Mbarak  Abdulwakili   amewataka  wateandaji  kujenga  utamaduni  wa  kuwaeleza   wananchi  ukweli   kwa  mambo  yanayowezekana  na yasiyo wezekana  ili  wasipoteze  muda  n a  kwa  yale  yaliyoko nje  ya uwezo wao wayafikishe mapema  panapohusika .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment