Image
Image

Kenyata atia saini muswaada wenye utata wa kupambana na Ugaidi




Rais UHURU KENYATTA wa Kenya ametia saini muswada wenye utata wa sheria ya kupambana na ugaidi
ambao wakati wa mjadala wake bungeni ulizusha vurugu na wabunge kurushiana makonde,
Muswada huo ulipitishwa na Bunge katika kikao kilichokumbwa na ghasia huku Wabunge wa upinzani
wakionya kuwa Kenya ilikuwa inageuka kuwa taifa la polisi huku serikali ikisema inahitaji mamlaka zaidi ya kupambana na wapiganaji wa kiislamu wanaotishia usalama wa nchi hiyo.
Kupitishwa kwa muswada huo na kutiwa saini kuwa sheria na Rais KENYATTA kunakuja wakati wapiganaji
wa Somalia wa kikundi cha al-Shabaab chenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani al-Qaeda kikizidisha mapigano nchini Kenya na kuua watu 64 katika mashambulio mawili ya hivi karibuni kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Mapema mataifa tisa ya nchi za magharibi yaliunga mkono sheria hiyo lakini yakataka serikali ya Kenya iheshimu haki za binadamu huku wapinzani wakisema sheria hiyo itawanyima watu uhuru na haki zao na
kuvibana vyombo  vya habari.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment