Image
Image

Kuwasili kwa vifaa ndio kutakapo wezesha kukamilika kijiji cha Dijital Nchini Tanzania



Mwandishi wetu, Arusha
Ndoto ya kuwa na kijiji cha dijitali nchini Tanzania itaanza kutimia Januari
mwakani wakati vifaa vinavyotakiwa kukamilisha mradi huo vitakapowasili
kutoka kampuni ya Samsung Electronics.
Kwa mujibu wa watekelezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kutumia dola za Marekani milioni 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)  vifaa hivyo vinatarajiwa kuingia Bandari ya Dar es Salaam Januari tano  mwakani.
Mkataba wa kuanzishwa kwa kijiji cha dijitali eneo la Ololosokwan tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro ulitiwa saini kati ya Unesco na Samsung electronics Novemba 6 mwaka huu.
Akizungumza  na halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan ,Mkurugenzi Mkazi wa Shirika  la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues amewataka wanakijiji kujiandaa  kwa mabadiliko makubwa ya kijiji chao kinapoingia katika dunia ya  dijitali. 

Alisema mambo ambayo wanastahili kuyaweka sawa ili kufanikisha ndoto zao
kuhakikisha eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi ipo ni lazima
lisajiliwe kisheria ili kusiwepo na tatizo katika siku za usoni.

Aidha kutokana na ukubwa wa mashine zinazohusika, hasa makontena ni vyema  wanakijiji wakaangalia maeneo korofi katika barabara za kuelekea huko na kuzirekebisha, ili magari hayo makubwa yenye vifaa yapite kwa usalama.
Alisema mradi huo wa miaka mitatu unatarajia kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kuwa na ujasirimali, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika mawasiliano na utafutaji wa masoko, elimu na afya.
Kwa mujibu wa Bi.  Rodrigues kijiji hicho pia kitakuwa na shule iliyoungwa na mtandao wa kompyuta duniani (intaneti), kliniki ya kisasa, tiba kwa kutumia  teknolojia ya kompyuta na jenereta kubwa linalotumia nishati ya jua. 

Aidha
kuwapo na mtandao wa kompyuta kutawezesha UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzisha mtaala utakaowawezesha vijana wa kimasai ambao ni wafugaji kupata elimu wanayoihitaji.

Mwakilishi huyo wa UNESCO amesema kwamba amefurahishwa na namna watu  walivyoitikia mradi huo ambao umelenga kubadili maisha ya wafugaji hao  kwa kuwawezesha pia kuitumia vilivyo sekta ya utalii.
“Kupitia  mradi huu wananchi wanaweza kujifunza kusoma, kupata maarifa na katika  harakati hizo kujua lugha ya kiingereza ili kuwasaidia kuwa na
mawasiliano na watalii na watu wengine”, alisema Rodrigues. 

Alisema ni nia ya Unesco kuhakikisha kwamba inasaidia kufuta ujinga miongoni  mwa wafugaji hao bila kuathiri utamaduni wao wanapoingia katika maisha  ya kisasa.
Kijiji cha digitali cha Ololosokwan kitakuwa cha nne
barani Afrika na yapo makubaliano ya msingi kwamba kijiji kingine
kitajengwa Zanzibar mwakani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment