Image
Image

Nchi za Kiafrika zatakiwa kupambana na Ebola



Waziri Mkuu wa Ethiopia amezitaka nchi za Kiafrika kujiimarisha zaidi katika mapambano dhidi ya homa ya Ebola, badala ya kutegemea zaidi misaada kutoka madola ya Magharibi.
Hailemariam Desalegn amesema kuwa, mapambano dhidi ya homa ya Ebola barani Afrika hayapaswi kuachiwa madola ya kigeni. Desalegn amezitaka nchi za Kiafrika kuitikia wito wa Umoja wa Afrika wa kupelekwa madaktari na wafanyakazi wa sekta ya afya kwenye maeneo yaliyokumbwa na homa hiyo hatari ambayo hadi sasa haijapatiwa tiba wala chanjo.
Waziri Mkuu wa Ethiopia amesisitiza kuwa, nchi za Kiafrika zinapaswa kuonyesha kuwa zina umoja na mshikamano. Desalegn ameongeza kwamba, Waafrika wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwenye operesheni za utoaji misaada barani humo.
Wiki iliyopita Ethiopia ilipeleka madaktari na wafanyakazi wa sekta ya afya wasiopungua 187 katika nchi zilizoathiriwa na Ebola za Sierra Leone na Liberia.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment