Image
Image

Wabunge kenya watofautiana wakati wa mjadala juu ya muswaada.




Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wa kenya.
Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo. 
Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'
Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.

 BBC

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment