Image
Image

Zambia yatetea shirika lake la habari kufuatia shutuma za kuonyesha upendeleo kwenye uchaguzi wa rais



Serikali ya Zambia imelitetea shirika lake la habari ambalo limekuwa likilaumiwa kwa kuonyesha upendeleo kwa baadhi ya wagombea urais kwenye uchaguzi wa Januari 20 nchini humo.
Shirika la Habari la Zambia ZANIS limekuwa likilaumiwa na wapinzani na mashirika ya kijamii kwa kuweka vifaa vyake vya matangazo kwenye uteuzi wa mgombea wa ugavana wa chama tawala Bw Edgar Lungu. Tume ya uchaguzi ya Zambia imetaja hatua hiyo kama inayompa Bw Lungu nafasi kubwa ya ushindi dhidi ya wapinzani wake na kusisitiza kuwa huduma hiyo inatakiwa kutolewa kwa kila chama cha kisiasa.
Hata hivyo msemaji wa serikali Bw Joseph Katema amepinga madai hayo na kusema kitendo hicho hakikukiuka sheria za uchaguzi kwa kuwa kaimu rais Bw Guy Scott alikuwa miongoni mwa watu waliomsindikiza Bw Lungu kuwasilisha makaratasi yake ya uchaguzi.
Jumla ya wagombea 11 wamejitosa katika kinyang'ang'anyiro cha urais wa Zambia kufuatia kifo cha rais wa zamani Bw Michael Sata Oktoba 28.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment