Image
Image

Breaking News:Mafuriko Mtwara yasababisha maafa


Kwa habari ambazo zimefikia Tambarare halisi muda  zinasema kuwa nyumba kadhaa zimezolewa na maji na kusababisha mafuriko mtwara mjini na kusababisha maafaa na kuharibu miundombinu mbali mbali kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo.

Kufuatia maafa hayo, Kamati ya Ulinzi na Usalalama ya mkoa wa Mtwara imeanza thathmini ya athari ya mvua hizo zilizoanza kunyesha kuanzia alfajiri ya leo. 
Wakati huo huo Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA anatarajiwa kuwasili Mtwara kutembelea eneo la Msimbati wilaya ya Mtwara Vijijini kujionea uharibifu uli o tokana na  ongezeko la kina cha maji ya   bahari kilichosababisha kumezwa kwa  sehemu ya ardhi yenye ukubwa wa mita mia   moja na sita . 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara HALIMA DENDEGU amesema mara atakapowasili Mheshimiwa PINDA ataelekea eneo la Msimbati ambalo liko kilomita 60 kutoka mtwara mjini. 
Kuhusu maendeleo ya kudhibiti kingo za maji ya bahari Mkuu huyo wa mkoa amesema kazi hiyo inaendelea vizuri ingawa ni ngumu kutokana na maji hayo kuhamia sehemu nyingine na kufanya uharibifu. 
Hata hivyo amesema sehemu kubwa ya kingo za bahari zimefanikiwa kujazwa mawe na mchanga kwa wingi hatua ambayo ni ya awali ili kudhibiti mvua kubwa ambazo zilitabiriwa na mamlaka ya hali ya hewa ya kuwapo kwa mvua kubwa katika mikoa ya kusini siku ya leo.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment