Image
Image

Mtu mwenye bastola feki avamia kituo cha runinga asitisha matangazo ya TV nchini uholanzi


 Mtu huyo akiwa amenyanyua mikono baada ya polisi kuingia studio
Mwanaume mmoja aliyekuwa na bastola feki, amekamatwa baada ya kuvamia studio za kituo cha televisheni ya taifa ya Uholanzi ya NOS, na kupelekea taarifa ya habari ya usiku kutorushwa.
Mwanaume huyo aliyevalia vizuri akiwa ameshika mkononi bastola hiyo refu yenye kiwambo cha kuzuia sauti, alifanikiwa kupenya na kuingia studio, na kushinikiza apewe muda wa kuongea hewani.
Kufuatia tukio hilo kituo hicho cha TV cha NOS, kililazimika kuzima matangazo yake kwa muda wa saa moja,lakini kamera ziliendelea kumrekodi mwanaume huyo hadi pale polisi walipofika na kumkamata.

    Polisi wenye silaha wakimsogelea mtu huyo 
Polisi wakimkandamiza chini ya sakafu mtu huyo ili kumfunga pingu
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment