Image
Image

Ratiba ya wizara ya Elimu yakinzana na ratiba ya NEC yawabana wanafunzi kutopiga kura uchaguzi mkuu ujao.


Kasumba  ambayo imekuwa ikijengeka mara nyingi  na inazidi kujengeka kwa wanafunzi mbali mbali nchini juu ya inapofikia kipindi cha kupiga kura katika uchaguzi mkuu hatimaye inaelezwa kuwa zaidi ya wanafunzi laki sita wa vyuo vikuu, vyuo vya kati na kidato cha nne nchini huwenda wasishiriki katka zoezi zima la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao wa madiwani,wabunge na Rais kutokana na ratiba ambayo imetolewa na wizara ya elimu kuhusu mihula ya kufunga na kufungua vyuo nchini kukinzana na ratiba ya tume ya uchaguzi nchini, NEC.

Kutokana na hofu hiyo, CHASO imeandikia waraka na kuelekeza katika ofisi ya katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ikimtaka kuwatumia wabunge wake kupeleka hoja binafsi Bungeni ya kurekebisha sheria ya uchaguzi ili iwaruhusu watanzania wote kupiga kura wakiwa mahali popote ndani ya mipaka ya Tanzania.
Ratiba ya mihula ya kufunga na kufungua vyuo ambayo imetolewa na wizara ya elimu mwaka huu, imeibua hofu kwa wasomi wa vyuo mbalimbali nchini kutoshiriki ipasavyo kwenye uchaguzi mkuu ujao, ambapo jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHASO) Mkoani Mbeya wamelibaini hilo na kuanza kupaza sauti zao kuidai haki hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment