Image
Image

Yaliyokuwa yakijiri bungeni mjini Dodoma Leo


Swali- Zungu: Kuhusu sera ya mkurabita ambayo imeigwa mpaka Kenya na Wenzetu wanakusanya mpaka Tsh trillion 8. Nchini kwetu bado wafanyabiashara wadogowadogo wananyanyaswa kila kukicha, Tunakuomba Mamlaka zako zikae na wadau ili wafanyabiashara hawa wafanye biashara kwa amani ndani ya nchi yao, Tunaomba kauli ya serikali
Jibu- Waziri mkuu : Katika mazingira yetu ni vizuri mamlaka za mikoa na wilaya zishirikishe wadau hawa, mimi naamini yote yanaweza kurekebishwa kwa kupanga pamoja na kuweka mipango mizuri. Huu utaratibu upo hata ulaya. Natoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kukaa na vijana na kupanga nao taratibu hizo. Kwa upande wa ilala tutakaa pamoja mimi na wewe mbunge wao na wadau wengine ili tuweke mipango ya pamoja.
Swali la nyongeza: Usafi wote tunaupenda lakini zoezi linaloendelea sasa hivi ni unyanyasaji wa wanyonge. Watu kuporwa mali, hawa vijana wanategemewa na majukumu, nakuomba waruhusiwe kufanya biashara zao mpaka saa kumi pale kariakoo.
Jibu: Nakubaliana na Wazo lako, na wale wote waliohusika kwenye unyanyasaji wachukuliwe hatua
Swali- Halfani Hilali: Kuhusu sera ya serikali ya kilimo kwanza, na kilimo bila ardhi hakipo , kumekuwa na mgogoro wa Ardhi wilaya ya Sumbawanga, malonje na serikali bado haijatatua mgogoro huu, nini kauli ya serikali kwenye mgogoro huu.
Jibu: Ni kweli mgogoro huu haujaisha ila serikali inafanya jitihada za kuimaliza mapema.
Swali- Ngonyani: Mwaka 2015 ni mwaka wa uchaguzi mkuu, Mji wa mombo uliomba kuwa almashauri na serikali ilikagua na kuona vigezo vyote vimekamilika.
Jibu: Naomba unipe muda nifatilie nitakupa jibu.
Swali- Mnyaa: Kuhusu NIDA Na Vifaa vya Biometric.
Majibu yametolewa na waziri Mkuu.
Wameuliza Maswali watu sita tuu;
MASWALI YA KAWAIDA- OFISI YA WAZIRI MKUU
Swali- Mbowe: Mh Spika, katika majibu ya waziri anashauri almashuri zitenge fedha za kutosha kwenye kuondoa taka wakati anajua hali ya kiuchumi kwenye almashauri zetu ni mbaya, kwanini serikali isiweke comitment ya kubadili taka hizo kuwa mali na kutumika kwa shughuri zingine? 
Jibu: Kwenye sheiria ya mazingira ya mwaka 94 inaelekeza kila almashauri iingize maswala ya usafi kwenye mikakati yake ya maendeleo. Lakini shughuri za rescycling zinafanyika na zinaruhusiwa.
OFISI YA RAISI UTAWALA BORA
Swali la Mh Merriam Msaba: 
Jibu: Serikali inayo mamlaka ya kupokea matamko ya watumishi wa umma, tathin iliyofanyika mwaka 2013 inaonesha zaidi ya 75% ya matamko yalikuwa sawa, na hivyo hakuna kiongozi aliyetoa matamko ya mali zake ambazo ni za uongo. 
Swali la nyongeza: Kunaviongozi na wafanyabiashara wakubwa wamewekeza fedha zao hapa na watanzania wamenufaika. Moja kwanini viongozi wanaowekeza fedha zao nje ya nchi wasiwekeze ndani ili taifa linufaike?
Majibu- Naibu waziri: Zipo sheria za kuzuia na kupambana na rushwa inasema iwapo mtumishi wa uma anagundulika kupata mali zisizo za halali basi mali zake zinaweza kutaifishwa na pia anaweza kufunguliwa mashtaka na tayari kuna zaidi ya kesi tano mahakamani.
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO
Swali moja.
WIZARA YA FEDHA
Swali La Kigwangala.
Jibu: Chanzo kikuu cha mapato ya serikali ni Kodi, ni kweli wananchi wanachangia malipo kwenye baadhi ya huduma zinazotolewa na serikali, kwa gharama ndogo sana ukilinganisha na mahali pengine. Serikali inatoa Elimu ya sekondary bure japokuwa kuna mchango kidogo unaotolewa na serikali.
Swali la nyongeza: Kwanini serikali iliyopewa mkataba na wananchi ya kutoza kodi na kusimamia maendeleo kwanini serikali iendelee kuchangisha wananchi tena kwa kutegemea michango ya wahisani wakati inakusanya kodi ?
Jibu- Naibu waziri: Bajeti yetu bado ni ndogo kwahiyo serikali yetu inahitaji vyanzo vingine vya mapato ili kukidhi huduma hizo. Bado serikali itaendelea kutegemea michango ya wahisani na ya wananchi ili kukidhi huduma.
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Swali - Mh Shabiby: Kuhusu Mradi wa REA:
Jibu Naibu waziri nishati na madini: Serikali imeagiza miradi yote ya umeme ikamilike ifikapo mwezi juni mwaka huu.
Swali la nyongeza: Kwanza siridhiki na haya majibu, kwakuwa ninauhakika kuwa mkandarasi hajasaini mkataba kwenye haya maeneo, Je mpo tayari twende Gairo kuhakiki kama wamesaini?
Majibu: Tutaenda jumamosi kuhakiki kama kazi hiyo inaendelea, TANESCO ndio mnajukumu la kutekeleza miradi hii ya REA kwahiyo ihakikishe inashirikiana vizuri na wabunge wa maeneo husika.
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Swali la nyongeza- Mbatia: Wanawake wanaojua kusoma na kuandika ni 75.5% tu, huoni kuwa Tanzania tumerudi nyuma kwenye malengo ya millenium kwa zaidi ya 20% ukilinganisha na mahali tulipokuwa kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita?
Majibu- Waziri: Ni kweli hali ya kutokujua kusoma na kuandika kama taifa hatujaridhishwa, lakini kama taifa tumepika hatua nzuri, kwa mkoa wa mwanza idadi ya wanaojua kusoma na kuandika kwa wanawake idadi imepanda kwa asilimia 10. Tupo tayari kutumia media ili kuwaelimisha waliokosa nafasi ya kusoma.
WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI:
Swali la nyongeza Mh Mtangi: Katika shamba la mkonge la Bwembwela, Kulikuwa na Matatizo, Je migogoro huo umeisha kabla ya kuanza ugawaji wa shamba hilo?
Swali la pili, Utaratibu gani ulitumika kufuta hati za shamba la Bumburu?
Majibu- Naibu waziri: Mheshimiwa raisi alitoa maagizo kuwa almashauri ihakikishe hakuna mgogoro wa kisheria kabla ya kfuta hati. Kwenye swali la pili naomba muda nifatilie nitakuletea majibu.
WIZARA YA HABARI
Swali- Mohammedi Ibrahim : Ni lini magazeti yatapunguza bei ili wananchi waweze kupata habari?
Majibu- Naibu waziri: Bei za magazeti zinatehemeana sana na gharama za uzalishwaji.
Swali la nyongeza: Haoni kuwa serikali inatakiwa kupunguza kodi ili bei za magazeti zipungue na kila mwananchi aweze kupata habari ?
Swali la pili: Serikali kwanini isipunguze kodi kwenye Betri ili wananchi waweze kupata betri kwa bei nafuu?
Majibu- Naibu waziri: Serikali inahitaji kodi kwa ajili ya kuendesha taifa na kodi inayotozwa kwenye magazeti ni ndogo sana kwahiyo serikali haina mpango wowote wa kupunguza kodi.
Swali la nyongeza- Mbilinyi: Kuhusu kufungiwa gazeti la ----
Majibu: Gazeti lilifungiwa kwa muda usiojulikana, kwahiyo kufunguliwa kwake kunategemea mapenzi ya serikali, Tanzania ni yetu sote naomba waandishi wazingatie maadili ya taaluma zao.


 KIPINDI CHA MASWALI NA MAJIBU KIMEISHA. SPIKA ANATANGAZA WAGENI WALIOTEMBELEA BUNGE
Wamachinga na mamalishe Wakiongozwa na Mh Lusinde Wametembelea Bunge Leo
Matangazo ya vikao vya kamati za bunge, yanatolewa na spika
HOJA YA KUJADILI JAMBO LA DHARULA LILILOTOKEA (Hoja ya Mbatia kwa muujibu wa kifungu cha 47)
WAZIRI YA MAMBO YA NDANI MAELEZO YA SERIKALI KUHUSU HOJA YA MBATIA
"Kufatia hoja ya Mh James Mbatia Mbunge ninamaelezo yafatayo, Tar 26 Jan Jeshi la polisi lilipokea barua kutoka Chama cha CUF. Barua hiyo ilikuwa ikitoa taarifa za kufanyika kwa maandamano kwenye viwanja vya Zackiem MBagara. 
Maandamano yalipangwa kuanzia Temeke kuelekea Zackiem, Jashi la polisi liliwaita viongozi wa CUF kwa mazungumzo. Walifanya mazungumzo na jeshi la polisi lilitoa tahadhari kadhaa kutokana na sababu za kiusalama. Viongozi wa CUF waliridhika na ushauri wa kamanda SIRO.
Tarehe 27 Jeshi la polisi lilipata taarifa za kuwepo kwa mkusanyiko mkubwa wa watu wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe tofautitofauti. 
Katika hali ya kushangaza Profesa Ibrahimu Lipumba alikaidi Zuio la Jeshi la polisi na Kuamrisha wananchi kuandamana kuelekea Zackiem. 
Kaimu kamanda wa polisi wa temeke alitangaza ilani na kuwaambia watu watawanyike kwa amani, Baada ya kukaidi ilani hiyo, jeshi la polisi lililazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji na kuwakamata.
Kutokana na matukio mengi ya ugaidi jeshi la polisi linapokea nakufanyia kazi taarifa mbalimbali kwa sababu za kiusalama.
Jeshi la polisi linataka kila mtu kutii sheria bila shuruti, Na mtu yoyote akishindwa kufanya hivyo jeshi la polisi litashughurikia mtu yoyote bila kujali umri, jinsia, wala madaraka yake.
Viongozi wa CUF walivunja sheria kwamakusidi ilikusaka umaarufu wa kisiasa na huruma ya wananchi, Tabia hii haitavumiliwa. VIongozi ni wajibu wetu kuungana kwa pamoja kulinda amani ya nchi yetu.
Vurugu zinapotokea hazichagui wa kumgusa, zinaweza kugusa watoto, wagonjwa na watu wengine na matukio hayo huwa hayatokei kwa makusudi.
Jeshi la polisi halitamuogopa wala kumhofia mtu yoyote yule, na ninawaagiza polisi nchini kote kufanya kazi yao bila hofu wala kumuogopa mtu yoyote yule kwa uadilifu.
Mwanasheria mkuu wa serikali:
 Jana wakati swala hili linaletwa Profesa Ibrahim Lipumba alikuwa hajafikishwa mahakamani, Kwamuujibu wa taarifa zilizotolewa, Professa Lipumba Alifikishwa Mahakamani Jana. Bunge hili tukufu linaongozwa kwa muujibu wa sheria na kanuni. Na kwa muujibu wa sheria zetu, bunge hili haliwezi kujadili jambo ambalo linasubiri uamuzi wa mahakama.
Jambo hili linaletwa bungeni ili bunge lijadili lifanye maamuzi, na limepelekwa mahakamani ili mahakama ilifanyie maamuzi. mamlaka yenye wajibu wa mwisho wa kutoa haki kwenye jamhuri ya muungano wa Tanzania ni Mahakama. Mheshimiwa spika naomba kushauri, kwenye mazingira kama haya bunge lako tukufu lisijadili jambo hili.
Kwa wananchi wa Tanzania ambao wanakumbu kumbu za kinachoendelea hapa nchini wanakumbukumbu jinsi nilivyokuwa mstari wa mbele kutetea mamlaka ya bunge yalipokuwa yanataka kuingiliwa na mahakama kwa hiyo ni lazima tuwe tuna balance.
Spika anaruhusu hoja ijadiliwe kwa DK 3. 
Tundu lisu anachaguliwa kuwa mchangiaji wa kwanza, anapinga dk na kusema atatumia dk 15 zilizopo kisheria.
Spika anatoa dk 10 badala ya 15 alizosema awali.
Tundu Lissu: Mrithi wa Warema ni mwanasheria mkuu wa serikali na sio mwanasheria mkuu wa Bunge kwa hiyo. Kwa maneno hayo ya waziri yeye mwenyewe waziri huyo hastahiri kuendelea kuwepo kwenye kiti chake. Kwa maana hiyo ni Hata kauli ya wapigwe tu iliyotolewa na Mizengo pinda aliposema Wapigwe tu ilikuwa ni kauli ya Serikali na pia ni kauli ya chama cha mapinduzi. Kwahiyo Mtu mwingine ambaye hastahili kuendelea kuwepo kwenye nafasi yake muda huu ni waziri mkuu Mizengwe Pinda. 
Wengi wetu tunakesi za kusingiziwa na Jeshi la Polisi, Wananchi wanauwawa na jeshi la polisi. Katika mazingira haya Bunge lazima lichukue hatua. Na hatua ya kwanza ni kuwawajibisha hawa wenye mamlaka ya kisiasa wanaotoa amri ya kupigwa watu wasio kuwa na hatia.
Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo ya jeshi la polisi. Sheria zetu zitamke wazi kuwa watu wasizuiliwe kufanya maandamano. Nitatoa hoja kufanyika uchunguzi wa matukio yote ya mauaji yaliyofanywa na Jeshi la polisi.
Tume ya haki za binadamu, ilitoa kauli kuwa Jeshi la polisi inazuia mikutano halali ya siasa. 
Tanzania ni mahakama ya mahakama ya kimataifa ya Jinai Kwahiyo serikali isisahau jambo hilo.
Habibu Mnyaa:
 Pingamizi la jeshi la pilisi lilikuja siku ya Maandamano tar 27 asubuh, na sio tar 22 kama inavyosemwa. Kwahiyo ni swala la kusikitisha na la aibu Waziri kuja kutoa kauli za uongo hapa bungeni ni jambo la kusikitisha sana. Profesa Lipumba alitii kauli ya mahaka na Taifa zima limeshuhudia kwenye vyombo vya habari.
Mbali na kutumia nguvu zisizostahili, Jeshi la polisi lilitumia Zana zisizoruhisiwa kwenye kazi yao, Jeshi la pilisi lilitumia hadi wheel Spana.
Naomba Bunge lako tukufu lijadili na tuadhimie kulijenga jeshi la polisi liwe na madili. Jeshi lenyewe la polisi limegawanyika, Yapo mabo ambayo hadi majambazi yanaonekana yanatoka ndani ya jeshi la polisi. 
Ni jambo la kusikitisha, na wala sio kwamba tunapakaziana, na sasa tunahitaji refoarm ya jeshi la polisi, NI wabunge wangapi, wamekuwa wakikamatwa kwa amri za wakuu wa wilaya bila kuzingatia kuwa hadhi ya mbunge ni kubwa kuliko ya mkuu wa wilaya.
Kunamatukio zaidi ya 28 ya mauaji yaliyofanywa na jeshi la polisi kwamuujibu wa tume ya haki za binadamu. Kauli ya waziri mkuu ya kusema apigwe tu sio nzuri na haitumiwi tu na jeshi la polisi pekee.
Mkosamali:
 Kinachoendelea kwenye nchi yetu ni uvunjaji wa katiba, Ripoti ya common wealth (jumia ya madola) ilisema, Jeshi la polisi la Tanzania bado lina mifumo ya kikoloni ambayo lengo lake lilikuwa kuhakikisha Wakoloni wanabaki madarakani na waafrika hawaingii madarakani.
Leo mnachokifanya nyinyi CCM ni kufanya yeleyale waliyokuwa wanafanya wakoloni. Uchafu huu wa Polisi duniani huko wanaufahamu. Ili Jeshi la polisi liweze kubadilika nilazima sheria ibadilishwe kwa muujibu wa mapendekezo ya Common Wealth.
Kama mfumo wa jeshi la polisi utabaki hivi basi mauaji hayataisha. Jeshi la polisi kwa muujibu wa tafiti ndio taasisi inayoongoza kwa ulaji wa rushwa.
Nassari (dk 4): "Doller yoyote inayotumia nguvu na mabavu kutawala, inafundisha kuwa Nguvu hiyohiyo itumike kuiondoa hiyo doller" Nelson Mandella.
Hiyo inamaanisha, Nguvu mnayotumia kuwanyanyasa, wamachinga, wafanyabiashara, wanafunzi wa vyou na watu wengine maana yake ni kwamba mnawafundisha nao watumie nguvu hizohizo kuiondoa CCM madarakani.
Rashid Abdallah:
Tundulissu(Muongozo): "TBC imekatisha matangazo ili wananchi wasisikie mjadala huu, sasa mheshimiwa tunaomba kiti chako kitoe mwongozo"
Spika: "Mimi sina Taarifa"
Rashid Abdallah(Anaendelea):
 Jeshi la polisi linaendelea kufanya mauji Tanzania bila serikali kuchukua hatua yoyote. Lipumba anatakiwa kuheshimiwa kama kikwete. Waziri hafai kuendelea kuliongoza jeshi la polisi kwa kushadadia mauaji, waziri mkuu anashabikia mauaji, Serikali gani hii !!?
Mh Suddi: Naomba niweke kumbukumbu sahihi, kuwa watu waliopigwa risasi makusudi na jeshi la polisi nitawataja kwa majina. (Anataja majina ya watu waliouwawa kwa kupigwa risasa kwa wilaya zao).
Mapendekezo ya tume ya hashim Mbita kwanini serikali haiyafanyii Kazi? Tukio lililofanyika ni baya na halifai, Tume iundwe na jambo hili lichunguzwe ili likomeshwe. 
Mh Mbowe: Kwaza nasikitika kwa taarifa ya Kaka yangu Chikawe. Mara zote tukileta taarifa tunazozileta hapa bungeni huwa mnadharau. Mimi nilienda kumuona Lipumba polisi wakasema maelekezo ya kumkamata na kumpiga Lipumba wameyapata kutoka ngazi za juu.
Tar 13 Jun 2013, nilipigwa na Bomu, nikashambuliwa na mashine gard nikashambuliwa na bastola. waliokujwa kufanya uchunguzi, kwenye eneo lile kwa siku 3. Siraha hizo ni kwa muujibu wa Uchunguzi wa serikali. watu walikufa na kupoteza viungo, leo kwakuwa waliokufa sio watoto wenu mnashangilia.
Mbowe anaendelea kutoa mifano mbali mbali ya watu walioathirika kutokana na jeshi la polisi, anamsimamisha mbunge aliyepata kilema kwa mashambulizi ya jeshi la polisi.

Mh Shakifu: Jana ulifanya jambo la hekima kuahirisha bunge ili tuweze kusikiliza maelezo ya upande wa pili, Watanzania wanafurahia amani iliyoletwa na chama cha mapinduzi. Vurugu zinatokea kwasababu ya watu kutokuwa tayari kutii sheria za nchi.
Hekima na busara zinatakiwa katika kuhakikisha usalama wa wananchi. Kwanini unapozuiwa kufanya jambo ushindwe kutii? hakuna serikali itakayokuvumilia.
Nchi hii dhamana tumepewa chama cha mapinduzi. haiwezekani tuone wananchi wanateseka tukavumilia, tutapambana. Na mimi nakuomba waziri Chikawe uendelee na msimamo huo huo. Mimi napendekeza mh Waziri tume ya haki za binadamu iendelee kuchunguza.
Nawapongeza sana wabunge wa CCM kwa uvumilivu. sio halali kutaja mambo ambayo hujayafanyia uchunguzi, sisi ndio tumeshika dola, aiyetaka kufata utawala wa sheria afate na asiyetaka dola itaendelea kufata mkondo wake. Mimi nasema tuiheshimu serikali uchunguzi ufanyike.
Saidi Mkumba:
 Naomba nianze kwa kusema katika jambo hili kubwa lenye masirah ya kitaifa umoja wa wabunge ni muhimu. Wenzetu wengine wanataka kulifanya jambo hili liwe na masirahi ya kisiasa. kwenye jambo la masirahi ya kitaifa, tusihamishe jambo hilo kuwa la kisiasa. Ni kweli CCM imeunda serikali, na yanayofanywa na dola sio kweli kuwa ni amri za CCM. 
Nashauri waandishi wa habari, mheshimiwa spika kupitia serikali, waandishi wa habari wanatakiwa kiungia mahali popote pale. Nashauri waandishi wa habari tuwape vifaa vitakavyofanya watambulike wanapofanya kazi kwenye mazingira yoyote.
Swala la utii wa sheria ni jambo muhimu kwenye mazingira yoyote yale. Utii wa sheria ni jambo endelevu. Nawaomba wanasiasa wote tuheshimu jambo hili. Mimi nimeipokea taarifa ya waziri Chikawe, na ninaiunga mkono.
Yahaya Kassimu Issa:
 Busara zako ni za hali ya juu mh Spika, Viongozi tunahitaji busara na hekima, bila hivyo hatuwezi kuendeleza taratibu za viongozi. Leo tunazungumza vurugu za mwaka 2011 inabidi tujiulize ilikuwaje !? Sifikirii kama kunaserikali yoyote ipotayari kuona inatekwa. Pemba waliuana wenyewe kwa kishindo. Mimi mwanangu alikua askari nyinyi mlimchinja kama kuku na hakuna aliyekuja hapa kusema.
Kutafuta mabango ya maandamano yanaashiria uchochezi, yalitokea mambo hayo Magomeni mbona hamkuonekana !? Sio kila aliyendani ya serikali ni mwanachama cha mapinduzi na ndio anayefanya mabaya.
Na kwanini kilasiku iweka CUF na CHADEMA tu!
Sound Over "Imekuuma eeh! Chomoaaa"
Aibu hii mnayoleta mnatupa sisi tunao ongoza nchi, Nani atawatetea askari katika nchi hiii ? Juzi tanga askari amepigwa hakuna aliyekuja kusema, watu hawalali kutulinda leo tunakuja kuwasema humu bungeni, maana yake nini !! Jiheshimu ili uweze kuheshimiwa usipojiheshimu hakuna atakaye kuheshimu,
Mh Sadifa (Mwenyekiti UVCCM): "Maalimu Seif alisema mwaka huu tutamwaga Damu, na ndio hili tunaloliona" Haki ya kuandamana ipo kikatiba na imezungumzwa kwenye kipengele cha 30 (ananukuu +sub article 2). Hakuna haki isiyokuwa na mipaka, Kwamuujibu wa sheria na taratibu za nchi.
Polisi walichotumia ilikuwa ni resonable force, Mimi nawaomba Tundulisu na Mkosa Mali wasome vipengele vyote vya sheria wasisome badhi tu ya vipengele. Nawaomba vijana wenzangu wasikubali kutumika na wanasiasa wamechoka. 
Na Waziri mkuu hawezi kujiuzuru kwasababu Mh Lipumba Kaguswa tu, Lipumba hajapigwa kaguswa tu. Na msimfananishe Lipumba na Kikwete, CUF sio chama ni SACCOSS tu.
Sound Over (Mtoto sio Rizki).
Mh Lussinde: Lazima wabunge tuheshimiane, kwanini mbunge mwingine akiongea wengine mrushe maneno. Lipumba sio wakwanza kupigwa !? Tena nalipongeza jeshi la polisi kwa kumpiga Lipumba ndio inavyotakiwa kwasababu wamempiga muusika, sio wanavyofanya kupiga watu wengine wa pembeni.
Wanasiasa wakae wakijua kuwa ukipenda boga penda na ua lake. Mimi nawaasa wanasiasa wote tushirikiane kulinda amani bila kujali vyama vyetu.
Kwanini ubishane na polisi !! Wapinzani ndio kazi yao kushauri tujiuzuru. Tusitengeneze vikundi vya janjaweed, Upinzani wanaona kilakitu kinachofanywa na serikali ni kibaya, polisi hawawezi kuchekea uhalifu.

Nawashauri polisi kwenye maandamano wapige wahusika.
Mtoa hoja Mh Mbatia anakamilisha hoja yake.
Mh Mbatia: Mmeikimbiza hoja mahakamani ili bunge lisifanye kazi yake. Hakuna mwenye mamlaka ya kumwaga damu ya mtu, hicho ni kitendo cha kigaidi. 
SAUTI IMEKATIKA BUNGENI (3dk)
Mbowe(anaendelea): Vyombo vya habari vilionesha wakinamama wakipigwa bila huruma, vitendo hivi vinaharibu sana umoja wa kitaifa, siamini kama kunachama kinashabikia uvunjwaji wa haki za binadamu. IGP Mwema alikiri ukiukwaji wa maadili ndani ya jeshi la polisi.
Tulikubaliana kufuta sheria kandamizi. Kitendo cha polisi kupiga watu wasiokuwa na hatia, kupiga wafanyabiashara kupiga wakinamama, kupiga wafugaji, sio kitendo kizuri. Jinai ni jinai haifutiki. 
Viashiria vyote vya kutoweka kwa amani vipo wazi, Jeshi la polisi linatumia mamlaka yake vibaya. Ms Spika bila kuegemea popote, hivi kweli umoja aliotuachia Mwalimu ndio huu ?
Nilimwambia Waziri Chikawe kuwa kuna uhuni ndani ya jeshi la polisi, angalia jinsi vituo vya polisi vinavyovamiwa, polisi wanachinjwa wanauwawa. Inabidi tuangalie sheria za zote zinazoiongoza polisi na kuzifanyia mabadiliko.
Vitendo vilivyofanyika ni vya kulaaniwa na sio vya kuungwa mkono kabisa na bunge hili.
MHESHIMIWA SPIKA
Anawashukuru wabunge kwa mjadala mzuri.
Waziri wa habari anatoa taarifa kutokana na kilichotokea: Anasema kuwa, kauli ya Tundu lissu sio kweli kuwa TBC ilikatisha matangazo yake.
SPIKA
: Saa 11 taarifa za kamati zitaletwa Bungeni. Spika anasitisha Bunge Mpaka Saa 11 jioni ya leo.
Cdt.J.F
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment