Image
Image

Lembeli awataka wananchi wa kahama na watanzania kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la wapiga kura

Mbunge wa Kahama, Mheshimiwa  JAMES LEMBELI amewataka wananchi wa Kahama na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga Kura baadae mwezi huu.
Amesema kujiandikisha kwenye daftari hilo ndiko kutawaweka tayari katika uchaguzi mkuu utakaowawezesha kuchagua viongozi bora wenye dhamira ya kweli ya kuwaongoza Watanzania.
Ameyasema hayo alipokuw akiwahutubia wananchi kwenye mkutano hadhara Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Mheshimiwa LEMBELI amesema Tanzania bado inahitaji viongozi bora wanaozingatia maadili ya uongozi na kushirikiana na wananchi katika kuiletea maendeleo Tanzania na hivyo njia pekee itakayowezesha kupatikana kwa viongozi hao ni kwa wananchi wengi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment