Image
Image

Makamu wa Rais aongoza maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es salaam katika maziko ya wana familia sita waliofariki Dunia baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto Kipunguni

Mama mzazi wa Kapteni David Mpila akiweka udongo katika kaburi la mtoto wake marehemu David Mpila  wakati wa maziko ya watu sita waliokufa kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia Februari 7 mwaka huu Kipunguni.


 Umati waombeleji ukiwa umejaa kwaajili ya kuaga ndugu na jamaa huku wengine wakionekana wameweka mikono kichwani wakilia wakati wakielekea makaburini kuwapumzisha wapendwa wao.
Wanafamilia wakiwa na huzuni baada ya miili kuwasili nyumbani huku wengine wakilia kwa uchungu kwa kupoteza ndugu na jama zao kwa wakati mmoja.
Miili ikishushwa kwenye gari baada ya ikiwasili nyumbani.
 Miili ikiombewa nyumbani kabla ya kuelekea makaburini kwa maziko.
  Makamu wa rais, Dk. Mohamed Ghalib Bilali akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyokuwa na miili ya watu sita wa familia moja waliofariki kwa ajali ya moto.
Mofisa wa Jeshi la wananchi wa tanzania (JWTZ) wakitoa heshima zao za  mwisho.
Majeneza yenye miili ya watu sita wa familia moja waliofariki kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto eneo la Kipunguni ‘A’ jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Februari 7, ambao walizikwa katika makaburi ya Airwing Ukonga, Dar es Salaam leo.
Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba moja ya jeneza la marehemu waliofariki katika ajali ya moto wakati wa maziko yao.
 Mtoto pekee aliyenusurika katika ajali hiyo, Emmanuel mpila akiweka udongo katika kaburi la baba yake, Kapteni mstaafu wa JWTZ, David Mpila.
 Mama mzazi wa Kapteni David Mpila akiweka shada la maua.
 Mama wa watoto wawili waliofariki katika ajali ya moto, Fatuma Issa akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake, Celina
 Baba wa watoto wawili waliokufa katika ajali ya moto, Emmanuel Mpila akiweka shada la maua katika kaburi la mmoja wa watoto wake, Pauline
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akiweka shada la maua kwenye kaburi kwa heshima.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick  akiweka shada la maua kwenye kaburi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiweka shada la maua.




 Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani akiweka shada la maua.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yenye miili ya Familia ya marehemu Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto nyumbani kwao Kipunguni, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji mama mzazi wa marehemu bibi Celina Mpila mke wa marehem Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam.  

           Simanzi kwa wapendwa wetu.

MAKAMU wa Rais Dkt.Gharib Mohamed Bilal,ameongoza maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliojawa na simanzi katika mazikoi ya wanafamilia sita walifariki dunia  baada ya nyumba yao  waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto.

Maziko hayo yalifanyika katika makaburi ya Banana,Ukonga jijini Dar es Salaam,Waliofariki katika ajali hiyo ya moto na kuzikwa jana ni Mzee David Mpila, Selina Mpila, wajukuu wawili Selina na Paulina, mtoto wa Mpila Lukas na shemeji wa Mpila.

Akizungumza katika maziko hayo Dkt.Bilal aliwataka Watanzania kuweka vizimia moto katika nyumba zao ili kujiepusha na majanga ya moto kama hayo yaliyotokea katika familia ya marehemu Mpila.

Pia aliwataka kuweka madirisha yenye kufungua ili iwe rais kujiokoa pindi yanapotokea majanga ya moto,Aliwapa pole wafiwa na kuwaombea amani, nguvu na subira kwa Mungu kutokana na msiba mkubwa walioupata.

"Msiba huu si wenu peke yenu bali ni msiba wa kitaifa na ndio maana na sisi tupo hapa kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja katika mazishi ya wapendwa wetu sina la kusema ila ninachokiomba ni Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi," alisema.

Naye, msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Mzingirwa, alisema tukio hilo ni tukio la kihistoria katika jimbo la Dar es Salaam, hivyo aliwataka wakristo waishi kwa amani na upendo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment