Image
Image

Rais wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi ameongoza mkutano wa magavana katika mji wa Aden, kusini mwa Yemen


Rais wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi ameongoza mkutano wa magavana katika mji wa Aden, kusini mwa Yemen huku akianza kutekeleza majukumu yake baada ya kutoroka kutoka kifungo cha nyumbani katika mji mkuu Sanaa. 
Kiongozi huyo anayeungwa mkono na nchi za Magharibi alikimbilia Aden Jumamosi iliyopita baada ya kutoka kisiri katika makazi yake mjini Sanaa ambako alikuwa akizuiliwa na kundi la waasi wa kishia wa Houthi ambalo linaudhibiti mji huo. Gavana wa jimbo la Aden Abdulaziz bin Habtoor amesema baada ya mkutano huo wa jana kwamba rais Hadi ataendeleza juhudi za kuiongoza Yemen kutoka Aden. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wakuu wa jeshi na idara za usalama.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment