Image
Image

Serikali mkoani mwanza imetangaza kiama dhidi ya wauaji wa albinism

Mlemavu wa ngozi  akiwa anaonekana na majeraha mbali mbali katika mwili na mikono yake baada ya kuwa amejeruhiwa na watu ambao wana wateka na kuwaua watu wenye ulemavu huo(Picha na Maktaba Yetu).>>> http://www.itv.co.tz/news
Serikali ya mkoa wa Mwanza imetangaza vita dhidi ya wahalifu wanaojihusisha na maua ji ya walemavu wa ngozi na kusababisha hofu kubwa kwa watu wenye UALBINISM  ambao wameshindwa kufanya kazi za maendeleo wakihofia usalama wa maisha yao baada ya kumeibuka kundi la wahalifu la kupora watoto wadogo wenye ulemavu wa ngozi na kuwachofoa viungo vya miiliyao kutokana na imani potofu za kishirikina.

Tamko hilo limetolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Mchungaji Baraka Konisaga wakati akizungumza na ITV katika hospitali ya rufaa bugando baada ya kumuona majeru hi aliyevamiwa na wahalifu nyumbani kwake katika kijiji cha ilelema kata ya ipalamasa wilayani chato mkoani geita BI.ESTER JONAS ambaye kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya rufaa bugando jijini mwanza.

Kwa upandewake mkurugenzi wa hospitali ya rufaa Bugando PROF KIEN MTETA amesema uongozi wa hispitali hautamtoza gharama za matibabu mgonjwa BI.ESTER JONAS na kwamba kumeanzishwa kampeni maaluma ya kuhamasisha jamii itambue umhimu wa kuwalinda walemavu wa ngozi ambapo muuguzi kitengo cha ent agineta mtatebwa amesema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri anaweza kukaa,kula chakula laini na kuzungumza.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment