Image
Image

Sumatra: Nauli za mabasi hazitashuka

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imeshikwa kigugumizi kuhusu suala la kushusha nauli ya magari ya abiria kwa kutoa sababu za kisheria pamoja na ukokotoaji wa tozo.
Ikasema, kwa mujibu wa Kanuni za Tozo pamoja na Sheria, Sumatra inapaswa kurejea tozo ya huduma baada ya mtoa huduma au mtumiaji wa huduma kupitia Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na Sumatra (Sumatra CCC) kuwasilisha maombi.
Pia huridhia viwango kwa kuzingatia masuala yote yanayoathiri gharama za uendeshaji, mafuta ikiwa ni moja ya eneo muhimu katika kukokotoa tozo zinazostahili kuridhiwa.
Meneja Mawasiliano kwa Umma, David Mziray alisema mwasilishaji wa maombi awe ni mtoa huduma au Sumatra CCC anapaswa atoe maelezo ya kina kuhusu sababu za kuomba mabadiliko ya tozo, jinsi alivyoathirika, ikiwa ni pamoja na kuambatisha nyaraka muhimu zinazoweza kuthibitisha hoja zake.
Alisema maoni ya wadau huzingatiwa kwa pamoja na masuala yaliyoainishwa katika Sheria ya Sumatra ambayo inatoa muongozo wa masuala ya kuzingatia katika kuridhia viwango vya tozo mbalimbali.
Alisema masuala hayo ni pamoja na gharama za uendeshaji, haja ya kukuza ushindani katika soko na kulinda maslahi ya watumia huduma na watoa huduma.
Akizungumzia kuridhia viwango kwa kuzingatia masuala yote yanayoathiri gharama za uendeshaji wanazingatia umuhimu wa kuwa na huduma endelevu, kulinda maslahi ya watumiaji na watoa huduma kwa kuweka mizania sawa na gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na mishahara na gharama za matengenezo.
Pia gharama za vipuri na matairi, gharama zaununuzi wa mabasi, riba kutokana na mikopo, gharama za bima, mafuta navilainishi, gharama nyingine za kiutawala, kodi na tozo mbalimbali, athari za viashiria vya kiuchumi kama mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi na kujenga mazingira ya ushindani.
Mziray alisema lengo la Sumatra katika kupanga nauli ni kuona pamoja na mambo mengine kuwa katika viwango vinavyoridhiwa kuna kuwa na ushindani zaidi miongoni mwa watoa huduma na hivyo kuwa na huduma bora zaidi na endelevu.
“Ni vyema kutambua kuwa kwa kiasi kikubwa huduma za usafiri wa umma zinatolewa na sekta binafsi, wengi wao wenye kipato cha kawaida. Hivyo basi nauli inayolipwa na abiria ndiyo inayolipia gharama za uendeshaji na kumpa mtoa huduma uwezo ili huduma iwe endelevu na kuvutia wawekezaji zaidi kuingia katika biashara hiyo,” alisema.
Alisema katika mazingira ambayo watoa huduma wamekuwa wakijielekeza katika kupata faida iliyokithiri, Sumatra imekuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mtumia huduma analindwa dhidi ya nauli kubwa kupita kiasi ambayo inaweza kumfanya mtumiaji huduma kushindwa kutumia huduma hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment