Image
Image

Watu wenye ulemavu mkoani GEITA wapokea msaada wa vyerehani ili kubuni mradi wa ushonaji nguo na kujikwamua kimaisha

Taasisi ya maendeleo ya VICTORIA FOUNDATION ya mkoani GEITA imekabidhi vyerehani Kumi kwa chama cha watu wenye ulemavu mkoani humo ili kukiwezesha chama hicho kubuni mradi wa ushonaji nguo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vyerehani hivyo Mkuu wa wilaya ya GEITA - MANZIE MANGOCHIE ametoa wito kwa taasisi nyingine nchini kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
Vyerehani hivyo vimekabidhiwa kwa kikundi cha walemavu mkoani geita na mkuu wa wilaya ya geita MANZIE MAGOCHIE na kutoa changamoto kwa kwa taasisi nyingine kuwasaidia watu wenye ulemavu.
Kwa upande wao baadhi ya watu wenye ulemavu mkoani geita hawakusita kuonyesha furaha yao baada ya kukabidhiwa vyerehani hivyo.
Katika hafla hiyo watu wenye ulemavu mkoani geita pia walipata fursa ya kujumuika katika chakula cha mchana walichoandaliwa na taasisi ya maendeleo ya victoria foundation.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment