Kaimu
Balozi wa Japan, Bw. Kazuyoshi Matsunaga akisoma risala fupi mbele ya
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini
mkataba wa msaada wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule
ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi
ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.(Picha zote na Zainul Mzige).
Baadhi
ya watendaji ofisi ya Waziri Mkuu waliohudhuria hafla hiyo fupi ya
utiaji saini mkataba wa msaada na Ubalozi wa Japan wa shilingi milioni
160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi
6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi (wa kwanza kushoto) akiwa na
watendaji wa mkoa wa Katavi na wilaya ya Mlele alioambatana nao kwenye
hafla hiyo fupi. Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo (wa pili
kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mlele, William
Mwakalambile (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mipango wa wilaya ya Mlele,
Seif Mohamed Makome (kulia).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia tukio la kubadilishana hati za mkataba
wa msaada baina ya Kaimu balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga
(kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mlele,
William Mwakalambile (kulia).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Japan mara
baada ya hafla ya utiaji saini wa mkataba wa msaada huo.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akifanya 'Power point presentation' ya hatua ya
ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni aliyoijenga kutokana na michango
ya wadau wa maendeleo kama kurudisha fadhila kwa jamii yake
iliyomsomesha kijijini kwake.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa
Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga (kulia kwake) baada ya kushuhudia
utiaji saini mkataba wa msaada wa Japan wa shilingi milioni 160 kwa
ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi na wapili kulia ni Katibu
Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Mlele, William Mwakalambile.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment