Image
Image

Licha ya jitihada za kuwanusuru walemavu wa ngozi zinazoendelea kwa juhudi kubwa Hatimaye mkoani Rukwa Mtoto mwingine atekwa na kukatwa mkono na watu wasio fahamika

Licha ya serikali na wananchi wake kupaza sauti zao kwa kukemea vitendo vya utekwaji Watu wenye ulemavu wa ngozi Albino lakini inaoyesha kuwa bado matukio ya ukatili dhidi ya albino yanaendelea kuwa tishio nchini Tanzania baada ya mtoto mwingine  wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono wake mkoani Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Shambulio hilo jipya limetokea  kwa mtoto wa kiume Baraka Cosmas wakati alipokuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto huyo anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.
Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino, Na muda mfupi baada ya Rais  wa Tanzania Jakaya Mrisho  Kikwete kupitia hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa pili mwaka huu  kukemea mauaji ya albino, ambao viungo vyao hutumika katika shughuli za kishirikina kwa imani potofu kuwa zinasaidia kuleta utajiri na madaraka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment