Image
Image

News Alert: Anusurika kifo baada ya gari kuteketea kwa moto katikati ya Coca Cola na Majembe Mikocheni jijini Dar es Salaam.


Na.Semvua Msangi,Dar es Salaam.
Mtu mmoja mwanamume aliyetambulika kwa jina la MUHIDIN SAID, mkazi wa Temeke Jijini Dar es Salaam,  amenusurika kifo jana usiku usiku baada ya gari alilokuwa akiendesha kuzima  ghafla na hatimaye kuteketea kwa moto katikati ya Coca Cola na Majembe Mikocheni jijini.

Akizungumzia chanzo cha moto huo SAID amesema wakati yupo kwenye gari alishangaa ghafla taa zimezima na hivyo ikamlazimu kushuka na kuangalia sababu za taa kuzima ndipo muda mfupi gari ikaanza kuungua.

Amesema huenda sababu ya moto huo ni hitilafu ya umeme kwenye gari.


Mwanamume huyo aliyenusurika kifo ana umri wa miaka 35 alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T944 BDE.

Amesema alikuwa na gari ya shemeji yake ambapo alikuwa akitoka Temeke akielekea Kawe kuirudisha ndipo baada ya matatizo hayo ilimbidi kupaki pembeni kabla ya kuendelea na safari na ndipo gari kuteketea kwa moto,kwenye gari hiyo alikuwa peke yake na hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa na hakuna kitu alichoweza kuokoa ndani ya gari hiyo dhidi ya maisha yake vitu vingine vyote viliteketea kwa moto.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment