Image
Image

Dk.Shei azindua mbio za Mwenge wa uhuru katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto)akimkabidhi  Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa Juma Khatibu Chum (kulia)  Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kulia)  Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge wa uhuru leo mjini Songea katika Uwanja wa Majimaji ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2015.


Mbio za  Mwenge wa Uhuru zimezinduliwa leo  katika mkoa wa Ruvuma ambapo Rais wa Zanzibar Dkt. Ally  Mohamed Shein  amewasha Mwenge huo katika uwanja wa majimaji mjini Songea  kwa ajili ya kukimbizwa nchini kote huku akiwataka wananchi kutoruhusu makundi yawayowagawanya.
Rais  wa Zanzibar Dkt Ally Mohamed Shein  akizundua mbio za Mwenge wa uhuru zilizopambwa na burudani  mbalimbali  amewataka wananchi kutoruhu makundi yanayowagawa.
Naye waziri wa habari ,utamaduni na  michezo  Dkt. Fenella Mukangala anataja ujumbe wa Mwenge wa uhuru ambapo  mkimbiza Mwenge kitaifa  awamu hi ni  Bw.Juma Hatibu Mchuma.
Naye mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu anasema Mwenge  utazindua,kuweka   mawe  ya msingi na kukagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni kumi mkoani humo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment