Image
Image

News Alert:Jinamizi la ajali bado laendelea kutesa wasafiri,basi la kampuni ya TAKBIR lavaana na ABOOD Mikese Morogoro.




Licha ya kupazwa sauti na wadau mbali mbali kila kukicha juu ya kutafuta mwarobaini wa kuweza kumaliza ajali za bara barani ama kupungua kabisa bado hali inaonekana kuchafuka kila baada ya iitwayo leo wimbo uliotawala midomoni mwa wananchi ni neon Ajali ili hali tukiwa mimi nawewe tukijiuliza Ajali ni nani,anatoka wapi,ni mtu ama upepo,ama nini ni haswa tusemapo ajali?.

Wakati kila mmoja wetu akitafakari hilo bhasi punde si punde navuta pumzi nasikia kama sauti ya kitu masikioni mwangu ambapo nilipokea ujumbe mfupi wa maandishi ukisema  Watu kumi na tano wamejeruhiwa na wengine zaidi ya hamsini wakinusurika kufa baada ya basi la kampuni ya  TAKBIR Lililokuwa likitokea mkoani geita kuligonga basi la kampuni ya ABOOD,maeneo ya Lubungo Mikese katika barabàra kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.

Idadi hiyo ya manusura bado ingali ikiturudisha nyuma kutafakari huyu aitwaye ajali ni nani?,wapo waliofunga, kusali na kuomba na hata kulazimika kukusanyika kwenye nyumba zao za ibada kumuombea huyu ajali atafunaye maisha ya watanzania kila itwapo leo bila huruma yoyote.




Ajali hii ambayo si nzuri  imehusisha basi aina ya SCANIA,mali ya kampuni ya TAKBIR lenye namba za usajili T.230 BRG,lililokuwa likitokea mkoani  Geita, kuelekea jijini Dar es Salaam, likiendeshwa na PROJETUS MODESTUS, mkazi wa mabatini mwanza ambalo kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,limeligonga  kwa nyuma basi la kampuni ya ABOOD  lililokua likitokea Morogoro kuelekea Dar es Salam likiendeswa na Abdala Hemed, mkazi wa kiwanja cha ndege Morogoro na kusababisha idadi hiyo ya majeruhi,wakiwemo wanawake wanane, wanaume watano pamoja na watoto wawili,huku dereva wa TAKBIR akidaiwa kukimbia baada ya ajali.



Nao majeruhi wa ajali hiyo wamebainisha chanzo cha ajali ni  dereva wa basi hilo kutokua makini na kuendesha gari kwa mwendokasi,na kwamba wanashukuru wanaendelea na matibabu, huku kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonard Paulo akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kutambua kuwa wanabeba roho za wananchi na hatma ya roho hizo  iko mikononi mwao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment