Image
Image

Serikali kutangaza bajeti ya fedha ya mwaka 2015/16.


Serikali inatarajia kutangaza bajeti ya shilingi trilioni 22,480.4 ya mwaka wa fedha 2015/16 ambapo shilingi trilioni 14 na bilioni mia nane zinatokana na vyanzo vya mapato vya ndani ya serikali kuu  na fedha zilizobaki zinatokana na mapato na mikopo yenye masharti nafuu kutoka nje na misaada ya wadau wa maendeleo.
Akiwasilisha mapendekezo ya mfumo wa mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2015/16  kwa wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, waziri wa fedha na uchumi Mhe.Saada mkuya amesema kati ya fedha hizo serikali itatenga shilingi trilioni 16 na bilioni 711.2 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, shilingi trilioni 6 na bilioni 612 kwa ajili ya mishahara taasisi na watumishi wa serikali ambapo fedha na miradi ya maendeleo imetenga shilingi trilioni 5 na bilioni 769.2 sawa na asilimia 25 ya bajeti yote.
Awali akisoma mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2015/16 waziri nchi ofisi ya Rais uratibu na mahusiano,Mhe Dkt Mary Nagu amesema katika mwaka wa fedha 2015/16 makadirio ya mahitaji ya fedha za kugharamia miradi ya maendeleo ni shilingi trilioni 6 na bilioni 279 ambapo shilingi trilioni 4 na bilioni 838 ni fedha za ndani na shilingi trilioni 1 na bilioni 441 ni fedha za nje na kusisitiza sehemu kubwa ya fedha hizo zimeelekezwa katika maeneo ya kipaumbele ya miundombinu,kilimo,viwanda,elimu,afya na maji.
Wakichangia mapendekezo hayo baadhi ya mabunge wamesema hayalengi kumletea maendeleo mwananchi wa kawaida changamoto zinazomkabili na hakuna unafuu wowote kwa kuwa imejikita zaidi kutegeme vyanzo  katika halmashauri ambapo huko hakuna uwekezaji wowote, huku wengine wakitaka serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya utalii baada ya kuonekana kwa miaka miwili mfulilo kuongoza katika kuiingiza taifa kimapato.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment