Image
Image

Sumatra imesema kuwa hakunasababu ya kuendelea kuwa na vitengo vya kuzuia ajali za barabarani kama ajali zitaendelea kupoteza maisha kila uchao.


Mamlaka ya kudhibiti  usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA imesema  hakuna  sababu ya kuendelea  kuwa na vitengo vya kuzuia ajali za barabarani kama  ajali  zitaendelea  kugharimu maisha ya watu na kusababisha vifo na vilema vya kudumu na kutaka vitengo hivyo   kama vimeshindwa  kazi  viachie ngazi.


Mkurugenzi wa mamlaka ya usafiri na nchi kavu na majini  SUMATRA Gilliard Ngewe ameyasem ahayo mkoani Morogoro wakati  akizungumza  na   wakuu wa jeshi  la polisi kitengo cha usalama barabarani kutoka mikoa yote nchini    pamoja wa maofsa wa SUMATRA na maofsa wateule wa halimashauri ambapo amesema siku hadi siku ajali za barabarani zimekuwa tishio  na zinajenga hofu kwa abiria  ambapo amezitaka mamlaka husika kuhakikisha zinakuwa na mpango madhubuti kwa ajili ya kupambana na ajali  hizo vinginevyo  hakuna haja ya kuw ana vitengo hivyo.
Mkuu   wa kikosi cha usalama bara barani  Mohamed Mpinga  akitoa taarifa  kuhusu hali ya ajali nchini anasema  ajali nyingi zimetokana  na makosa ya kibinadamu ambayo yamejumuhisha uzembe wa madereva matumizi mabovu ya barabara ambapo amesema jeshi la polisi litaendelea kujipanga na kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha ajali zinamalizika.

Katibu mkuu  TAMISEMI   Jumanne Sagini  amesema SUMATRA   na halmashauri nchini  zimefnaya makubalino  kutizama upya matumzi ya pikipiki  ambapo pamoja na kutoa huduma za usafiri  zinatumika vibaya kwa matukio ya uhalifu.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment