Image
Image

Thamani ya shilingi ya Tanzania yashuka kwa kasi kubwa yashtusha.


Kamati ya Bunge ya uchumi  viwanda na uchumi imeitaka serikali kutoa majibu kwa nini imepuuzia maagizo ya kamati hiyo hali ambayo imesababisha dola ya marekani kupanda na kufikia 2025 kutoka 1650 miezi mitatu iliyopita.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa  kamati hiyo Luhaga mpina amesema walitoa maagizo mengi kwa serikali ambayo yamepuuzwa hivyo siku ya alhamisi watatakiwa kuonana na kamati hiyo na kueleza kwa kina kuhusiana na  hali ya uchumi ilivyo hapa nchini.

Kwa upande wake waziri kivuli wa fedha James Mbatia amesema madhaifu yaliyopo nchini ikiwemo uingizwaji wa baadhi ya vifaa na vyakula vinavyoweza kupatikana hapa nchini navyo vimechangia hali hiyo hivyo ni bora taasisi ama watu wanaoagiza vitu ama vyakula kutoka nje ya nchi wakaacha kufanya hivyo.
Naye mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi nchini -TPSF Geofrey Simbeye amesema waliitahadharisha mapema benki kuu kuhusiana na mwenendo wa dola na kusema kuwa hali ilivyo sasa ni bora zikafanyika jitihada za dharura kuinusuru.
Juhudi za kuwapata viongozi wa benki kuu kuzungumzia kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya marekani inaedelea licha ya kushindikanika kwa siku tano mfululizo kwa madai kuwa wasemaji wa jambo hilo wapo katika vikao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment