Image
Image

Vituo vya mabasi ya mikoani vyakosa huduma za kijamii hali inayoweza kusababisha Magonjwa ya milipuko.

Asilimia kubwa ya Vituo vya mabasi hapa nchini Tanzania  vinadaiwa kukosa huduma za kijamii zikiwemo maji, maeneo ya kupumzikia abiria pamoja na huduma za vyoo zenye kukidhi haja ya wasafiri na watu wengine ndani ya vituo hivyo hali ambayo inaweza kupelekea kutokea kwa magonjwa ya milipuko.
Mkoani MBEYA baadhi ya watumiaji wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani wameilalamikia Halmashauri ya Jiji hilo kwa kuacha kukarabati jengo la abiria ambalo limechakaa na lina hatarisha maisha ya abiria.
Aidha imebainika pia kuwa kituo hicho kikuu cha mabasi kimekosa huduma za vyoo, na kuhatarisha afya za wasafiri na watu wanajishughulisha na kazi za kujiajiri kituoni hapo.
Akizungumzia changamoto hizo Mkuu wa wilaya ya Mbeya NYEREMBE MNASASABI amekiri kuwepo kwa changamoto ya kukosekana kwa huduma za choo kituoni hapo na kueleza kuwa ipo katika mpango wa muda mrefu wa serikali unaohusu kituo cha mabasi.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment