Image
Image

News Alert: Wanachama 150 wa Chadema warudisha fomu na kujiunga na CCM baada ya mbunge wa jimbo la kalambo kutoa msaada wa gari la kubebea wagonjwa.


Mbunge wa jimbo la kalambo Josephat Kandege amechafua hali ya hewa baada ya kutoa msaada wa Magari matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwenye  vituo vitatu vya afya vya Ngorotwa, Matai na Mwimbi wilaya Kalambo na hivyo kusababisha  wanachama 150 wa chama cha demokrasia na maendeleo  CHADEMA kurudisha kadi zao na kujiunga na CCM. 

Wanachama waliorudisha kadi ni wale wa Kijiji cha Kilewani, wilayani humo, ambao walifanya hivyo katika mkutano wa hadhara wakati mbunge huyo alipokuwa akihutubia kabla ya kukabidhi magari hayo kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama hao walisema lengo lao siyo kushabikia siasa bali kumuunga mkono mtu yeyote anayeweza kuwaletea maendeleo kama alivyofanya mbunge huyo.

Monica Sichalwe, alisema wameamua kurejea CCM kwa vile wanawake wilayani humo wamenyimwa nafasi ndani ya Chadema.
Awali akiwapokea wanachama hao, Mbunge Kandege alisema wote wanaojeruhiwa na vyama vya siasa wanakaribishwa CCM kwani huko ndiko uliko uhuru wa kweli na demokrasia.
Alisema wanachama hao na viongozi walioamua kurejea CCM wamepokelewa kwa mikono miwili na kamwe hawatajutia uamuzi wao.

Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kalambo Leopard Mbita alisema wakati huu CCM haipo tayari kuwafumbia macho wanachama na viongozi wake ambao ni tatizo hasa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu, kwani wanaweza kukikosesha ushindi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment