Image
Image

Batuli: Wazazi wanafurahia nguo za utupu.


MWIGIZAJI Yobnesh Yusuf maarufu kwa jina la Batuli, ameweka wazi kwamba tabia ya waigizaji wa kike kuvaa nguo za nusu uchi huwa zikifurahiwa na wazazi wa waigizaji hao.
Batuli alieleza hayo baada ya kuulizwa kwanini waigizaji wa kike wanapendelea mavazi ya nusu uchi wachezapo katika filamu zao.
“Hapo tatizo ni wazazi wa waigizaji hao wanaovaa nguo hizo wanaonyesha wanafurahia, kama wangechukizwa na tabia hiyo wasingevaa nusu uchi na kuiahibisha tasnia nzima na wanawake kwa ujumla,” alieleza Batuli.
Batuli mwenye ndoto ya kuasili mtoto wa kike, aliongeza kwa kuwataka waigizaji wenzake wavae mavazi ya kujitambua na yenye stara kwao, wazazi wao na jamii inayowazunguka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment