Image
Image

Hamad Rashid: Nec hakikisheni kila anayestahili anaandikishwa.

Mlezi wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Hamad Mohamed Rashid (pichani), ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( Nec), ihakikishe Watanzania wote wenye sifa wanaandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Hamad, Mbunge wa Wawi (Cuf) anayemaliza muda wake  na sasa amejiunga na ADC, aliyasema hayo wakati chama hicho kikikabidhi fomu kwa wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho. 
Alisema katika kipindi hiki ambacho uandikishaji unafanyika sehemu mbalimbali nchini kupitia mfumo wa Biometric  Voters Registration (BVR), kumebainika changamoto mbalimbali ambazo zinaashiria baadhi ya wananchi kushindwa kupata haki ya kujiandikisha.

Hamad alisema ni vema Nec ikafanya haraka kutatua changamoto hizo ili kutoa fursa kwa wananchi wote kujiandikisha.

Alisema hata katika maeneo ambayo kazi hiyo imekwisha malizika, lakini kuna watu ambao hawakuandikishwa, ni vema ikahakikisha nao pia wameandikishwa.

"Kazi ya uandikishaji katika daftari la wapigakura ni muhimu kwa mustakabali wa taifa, lakini mwaka huu imegubikwa na changamoto nyingi, idadi ya watu wanaohitajika kuandikishwa ni wengi na vifaa vilivyopo ni vichache," alisema na kuongeza:

"Ni rai yangu kwa Tume ihakikishe inatatua  haraka changamoto zinazojitokeza katika shughuli hiyo ili raia wote wa Tanzania wanaostahili wajiandikishe kwa kuwa ni haki yao Kikatiba."

Kadhalika, Hamad aliitaka Nec kusimamia na kutokwenda kinyume cha sheria za uchaguzi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Alisema Nec pekee ndiyo itasaidia uchaguzi huo uwe huru na wa amani endapo itasimamia sheria za uchaguzi ikiwamo kuepuka kuweka upendeleo kwa chama chochote cha siasa.

"Ninaiomba Tume katika uchaguzi huu, iepuke sana kupindisha sheria za uchaguzi kwa kupendelea chama chochote, inatakiwa kutenda haki kwa vyama vyote bila kujali ukubwa wake wala udogo wake na hiyo ndiyo njia pekee itakayosaidia uchaguzi huo ufanyike katika hali ya amani na utulivu.

Pia aliwaasa viongozi wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi mwaka huu, kuwasikiliza wananchi wa hali ya chini kwa kuhakikisha wanapatiwa haki zao za msingi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment