Image
Image

Kenya yatenga fedha dola milioni 5.3 kwa ajili ya wanamichezo wake watakoshiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Brazil.


Kamati ya kitaifa ya olimpiki nchini Kenya NOCK, imetangaza kutenga bajeti ya fedha dola milioni 5.3 kwa ajili ya wanamichezo wake watakaoshiriki mashindano ya olimpiki mjini Rio de Janeiro nchini Brazil mwaka ujao.

Kwa mujibu wa maelezo ya NOCK, fedha hizo zitatumika kugharamia mahitaji ya wanariadha 80 pamoja na timu mbili za michezo tofauti.

Kenya inapanga kutuma timu ya mchezo wa raga ya wanaume, na mojawapo kati ya timu ya taifa ya mpira wa wavu au ya soka ya wanawake.

Mwenyekiti wa NOCK Kipchoge Keino pia alitoa maelezo na kufahamisha kwamba wawakilishi kutoka nchini wamezuru Brazil kwa lengo la kusaka uwanja mzuri wa mazoezi.

Akizungumza katika sherehe ya uzinduzi wa shirika moja la misaada jijini Nairobi, Keino alisema, ‘‘Tuko tayari kwa maandalizi ya timu zitakazowakilisha Kenya. Tunahitaji fedha hizo kuanzia sasa ili kushughulikia wanariadha kati ya 80 na 100. ’’

Keino pia aliashiria mji wa Sao Paolo kuwa kama eneo mwafaka la kukita kambi ya mazoezi kwa wanamichezo wa Kenya kutokana na upungufu wa vifaa vya mazoezi katika mji wa Rio de Janeiro.

Katika mashindano ya mwisho ya olimpiki yaliyofanyika mjini London, Kenya ilituma jumla ya wanariadha 51 na kushinda nishani 2 za dhahabu, 4 za fedha na 5 za shaba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment