Image
Image

Lowassa kurudisha fomu Dodoma leo.

WaziriMkuu wa zamani Edward Lowassa,  leo anatarajia kurudisha fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukamilisha kazi ya kuwatafuta wadhamini.

Lowassa atarejesha fomu hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya  CCM  Dodoma baada ya kukamilisha kazi ya kusaka wadhamini 450 kutoka mikoa 15 ikiwamo mitatu ya Zanzibar.

Mgombea huyo alihitimisha kazi ya kusaka wadhamini juzi  mkoani Morogoro na jana alianza safari ya kuelekea Dodoma.
Akizungumza wakati akihitimisha safari yake ya matumaini Mkoani Morogoro ya kusaka wadhamini, Lowassa alisema kuwa tayari ameshapata wadhamini wa kutosha na wengine ataweka nyumbani kwake kama kumbukumbu.

"Nimezunguka mikoa yote 31 Tanzania bara na  Visiwani, nimepata wadhamini wengi hivyo nitapeleka idadi inayotakiwa 450 na haya mengine yatakuwa kumbukumbu ya maisha  yangu,"  alisema Lowassa.

Katika mikoa yote hiyo, Lowassa amepata wadhamini 874,297na alianza safari ya kutafuta wadhamini Juni 4, mwaka huu.
Katika ziara yake alikuwa akisisitiza wanachama kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili wakati ukifika wapige kura bila kupoteza haki yao ya msingi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Nec Idara ya Organaizesheni Muhammad Seif  Khatib tarehe ya mwisho ya kupokea fomu hizo ni kesho.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment