Image
Image

News Alert:HOFU-Uhalifu wa kutumia watoto wa zaidi ya miaka 10 KUIBA wabainika.


Askari wa jeshi la polisi wakionekana wakiwa kazini huku wakiwa wamejikok vitu mwilini kwaajili ya kufanya doria katika baadhi ya maeneo(Picha na Maktaba Yetu).
Jeshi la polisi maeneo ya Bunju nje kidogo ya jiji dar-es-salaam wamefanikiwa kuwanasa  watoto wawili wenye umri kati ya miaka kumi na kumi na mmoja na ambao hawajajulikana majina yao mara moja ambao wanasadikiwa kutumiwa na majambazi kuiba kwenye maduka ya huduma za simu na vipodozi huku watu wanaodaiwa kuwatuma kutoonekana hata baada ya kusakwa katika eneo hilo.
Askari akiwa kamshika mkono moja ya mtoto anayetuhumiwa kutumiwa na majambazi katika kufanya uhalifu.
Baadhi ya wamiliki wa maduka wamesema kuwa tukio hilo la limewashangaza watu wengi kwakuwa majambazi hao wametumia  mbinu mpya ya kukata dari la majengo hayo na kisha kuingia na kujificha katika dari wakisubiri wamiliki wa maduka waondoke jambo ambalo limezua hofu kwa wakazi hao.
Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya nyumba wakiangalia jinsi watoto hao walivyotoboa bati na kupenya ndani na kujificha kwenye dari kwaajili ya kufanya uhalifu.
Wananchi hao wameliomba jeshi la polisi kufika haraka wanapoitwa katika matukio lakini pia kushirikiana na vikosi vya ulinzi shirikishi kufanya doria mara kwa mara katika mitaa yao na kuwaondoa vijana wanaoshinda vijiweni na kutumbukia katika uvutaji wa bangi na uporaji.
Majibu ya wananchi wakizungumzia sababu namna watoto hao wanavyo tumika kihalifu wanaongea hapa#Bofya Kusikia,na kwa Taarifa Endelea kufuatilia Taarifa zetu kumbuka pia ku Like Page yetu hapo juu>>


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment