Image
Image

P Diddy Combs amesema kuwa hatakabiliwa na mashtaka.

Msanii wa muziki aina ya rap Sean P Diddy Combs amesema kuwa hatakabiliwa na mashtaka ya shambulio kufuatia kisa kimoja mwezi uliopita kilichohusisha uzani wa 'kettlebell'.
P Diddy aliye na umri wa miaka 45 alikamatwa mnamo Juni 22 kwa tuhuma za kushambulia kwa kutumia silaha hatari katika chuo kikuu cha California.
Alizuiliwa katika jela kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya dola 160,000.
Hakimu wa wilaya hiyo ameipeleka kesi hiyo katika mji wa Los Angeles kuamua iwapo Combs atakabiliwa na mashtaka hafifu.
''Tunafurahia kwamba hakimu alikataa mashtaka ya kutumia nguvu kupitia kiasi dhidi ya Combs'',alisema wakili wake.
Vyombo vya habari vilisema kuwa P Diddy alihusika katika mgogoro kati yake na kocha wa timu ya soka ya Marekani chuoni humo.
Hatahivyo Combs amesema kuwa alikuwa akimtetea mwanawe Justin Combs ambaye ni mchezaji wa timu ya chuo hicho na kwamba alikuwa akifanya mazoezi wakati wa tukio hilo.>>Bonyeza SHARE Hapo juu uwezavyo ili washkaji zako wasipitwe na Stori kama Hizi na Tunapokea matangazo maelekezo hapo kwenye ukurasa wetu yana jieleza kuwa wa kwanza kutangaza nasi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment