Image
Image

Raia mwenye asili ya ASIA akamatwa na mabegi ya fedha zaidi ya Shs.Milion 725 Dodoma.

Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mtu mmoja mwenye asili ya kiasia baada ya kukutwa  na mamilioni ya fedha kwenye begi akiwa kwenye Hoteli ya St.Gasper iliyoko mjini Dodom
Dereva wa gari lililokamatwa na fedha hizo Bw. Rashidi Shabani Nkungu mkazi wa Dodoma amesema alikodishwa na watu watatu wenye asili ya kiasia kutoka uwanja wa ndege kwenda Hoteli ya St.  Gasper iliyoko  mjini Dodoma.

Kwa upande wake meneja wa Hotel ya St. Gasper Bw,Denis Johanes amesema alibaini kuwepo kwa  jambo lisilo la kawaida baada ya maelezo aliyompa wakati anatafuta chumba kutofautiana na  aliyoandika kwenye kitabu cha wageni.

Alipotakiwa kueleza anakopeleka fedha hizo mtuhumiwa huyo pamoja na kukiri kuwa yeye ni mfanyakazi wa kampuniya Quality Group amesema alikuwa katika miamala yake ya kawaida.

Wakati jeshi la Poisi likiwa bado halijatoa ufafanuzi,kukamatwa kwa fedha hizo zinazokadiriwa  kufikia  zaidi ya milioni mia saba kumeongeza joto la wananchi na wana CCM wa mkoa wa Dodoma la kutoridhishwa na mwenendo wa matokeo ya vikao vinavyoendelea.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment