Ugonjwa wa Ukimwi unazidi kuwa janga
na mateso kwa wengi duniani kutokana na sheria zilizopo pamoja na
unyanyapaa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati
akizindua ripoti ya Umoja huo kuhusu Ukimwi huko Bridgetown, Barbados.
Ripoti hiyo iitwayo kushinda ukimwi na kusongesha mbele afya duniani
inatokana na mapendekezo kutoka kwa wataalamu wa afya, watu wanaoishi na
Ukimwi, vijana,wanaharakati na wadau wa umoja wa Mataifa.
Ban amesema sheria duni na unyanyapaa vinasababisha watu wengi
kutumbukia kwenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kukosa huduma za
matibabu za kuokoa maisha yao akinukuu takwimu za Umoja wa Mataifa kuwa
watu 250,000 huko Caribbean wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Mathalani amesema chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja zinatishia
haki zao za binadamu na haki za afya akisema jamii ya kimataifa haiwezi
kuvumilia ubaguzi huo kwa misingi ya jinsia ya mtu au utambulisho wake
wa kijinsia.
Halikadhalika ametaka kuzingatiwa kwa haki za makahaba na wale
wanaojidunga madawa ili kila mtu aweze kupata huduma dhidi ya Ukimwi
wakati muafaka.
Katibu Mkuu amekumbusha kuwa Ukimwi siyo tu suala la afya ya binadamu
bali ni suala la msingi la haki za binadamu na hivyo utatokomezwa pale
tu haki za msingi za kila mtu zitazingatiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment