Image
Image

Baada ya Daktari sasa Mourinho kuwabebesha Lawama Washambuliaji wake.


Katika Mchezo wa kwanza ufunguzi wa Ligi kuu Uingereza Chelsea ilitoka sare na timu ya Swansea. Matokea hayo hayakumfurahisha sana meneja mkuu wa timu hiyo Jose Mourinho ambapo moja kwa moja lawama nyingi alimtupia Daktari wa timu hiyo mwandada Eva Carneiro.

Mourinho alimshtumu daktari huyo kwa kupoteza muda wakati alipoenda kumtibu Mshambuliaji wake Ezen Hazard alipoumia dakika za mwisho.

Pengine daktari huyo hakuwa sababu ya Chelsea kukosa ushindi kwani mchezo uliofuata walifungwa 3 – 0 toka kwa Manchester City.

Chesea waliibuka na ushindi kwa mara kwanza kwenye mchezo wa tatu na waliwafunga West Brownch magoli 3 – 2 .

Mambo hayakuwa mazuri tena kwa upande wa Chelsea Lakini mwishoni mwa wiki baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Crystal Palace kwenye mchezo wao wa nne ndani ya ligi Kuu ys Uingereza.

Sasa kutokana na matokeo hayo, kocha Mourinho amewatupia zigo la lawama washambuliaji wake akiwemo Eden Hazard, Cesc Fabregas, Branislav Ivanovic na Nemanja Matic kwa kuwaita wazembe.

Mourinho amewapiga biti washambuliaji hao na huku akitishia huenda akawapunguza kwa kuwauza kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment