Image
Image

Duni haji atema cheche Mtwara*Asema UKAWA ikishika dola itafuta kilio cha wakulima.



Na.Sadick Juma,Mtwara.
Mgombea mwenza wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia ukawa Mh. Juma Duni Haji amesema hakuna sababu kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na lindi kuendelea kupunjwa bei ya zao hilo na serikali ya chama cha mapinduzi kwa kulipwa shilingi mia sita badala ya bei dira ya shilingi elfu moja iliyotangzwa msimu wa 2014/2015 na kuwahaidi watanzania kuwa UKAWA ikiingia madarakani itafuta mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umekuwa ukitumika kuwanyonya wakulima wa mazao mbalimbali nchini.

Akizungumza na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mtwara waliohudhuria mkutano huo wa kampeni za urais za vyama washirika vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi – UKAWA,zilizofanyika katika uwanja wa mashujaa mjini MTWARA – mgombea mwenza huyo amesema ikiwa watanzania wataipa ridhaa UKAWA ya kuongoza dola, watahakikisha wanafuta mfumo wa stakabadhi ghalani na kuboreshabei ikiingia madararakani.

Mapema akiwahutubia wananchi wa mji wa Newala,Mh.Juma Duni Haji pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa vyama vya NCCR – Mageuzi,chama cha wananchi ( CUF ) pamoja na CHADEMA, wamesema kuwa licha ya gesi kugunduliwa mkoani Mtwara,neema hiyo imegeuka kuwa mateso kwa baadhi ya wakazi wa mkoa huo huku ufafanuzi kuhusu kashfa ya RICHMOND ambayo imekuwa ikihusishwa na waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa ambaye kwa sasa ni mgombea urais wa CHADEMA kupitia ukawa ukizidi kuwekwa bayana.
Mgombea mweza wa UKAWA anazungumza hapa*Like Page na kuwa wa kwanza kusoma taarifa zetu .

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment