Image
Image

Maambukizi ya virus Ukimwi Kupungua licha ya Changamoto kadhaa.

Maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto  katika Mkoa wa Mtwara yamepungua kwa kiasi kikubwa, licha ya kukosekana kipimo kinachotumika kumpima mtoto ndani ya wiki nne hadi nane  bada ya kuzaliwa katika hospitali za wilaya.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mradi kutoka shirika lisilo la Serikali la EGYPAF, Dakta  PETER NAGUNWA katika ziara yake kwenye vituo vya afya vinavyotoa elimu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Amesema watoto wanaozaliwa na kina mama wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI wako kwenye hatari ya kupata maambukizi kutokana na hospitali za wilaya Mkoani  Mtwara kukosa kipimo anachotakiwa kufanyiwa mtoto.
Kwa upande wake Afisa Muuguzi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Ligula,  LUCY MKOREA amesema kwa kiasi kikubwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa  mama kwenda kwa mtoto yamepungua kutokana na elimu kutolewa kwa kiwango kikubwa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment