Image
Image

Wakulima wa korosho na wadau wakubaliana kwa sauti moja bei mwongozo kwa msimu wa 2015.

Mkutano mkuu wa wakulima wa korosho wakiwemo wadau wa zao hilo umemalizika wakiwa wamekubaliana kwa sauti moja bei mwongozo kwa msimu wa mwaka huu 2015-2016 ni Shilingi Elfu-Moja na 200.
Akitoa taarifa hiyo  kwa Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Bodi ya kurosho nchini,  ANNA ABDALLAH amesema  bei hiyo siyo ya soko bali korosho ipande ama ishuke mkulima atalipwa kiasi hicho cha pesa kwa kila kilo moja ya korosho.
Amebainisha kuwa msimu wa mwaka jana 2014-2015,  bei mwongozo ilikuwa Shilingi Elfu-Moja,  lakini bei ya soko kwa kilo moja iliuzwa Shilingi Elfu Moja na 400hadi  miatano bei ambayo amesema ilikuwa nzuri.
Amesema ana imani mwaka huu bei itakuwa nzuri hivyo amewaasa wakulima kuuza mazao yao kwa kutumia mfumo wa stakabadhi  ya mazao ghalani badala ya kukopa kwenye mabenki ambayo yamewarudisha nyuma  katika maendeleo.
Mkutano huo pia umetumika kuchagua bodi mpya ya wadhamini ambayo hushughulika na kukusanya michango ya wadau ambayo hutumika kugharamia shughuli za pamoja, na inafahamika  kwa jina la mfuko wa kuendeleza zao la korosho nchini.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment