Image
Image

Breaking News:Abiria waliokuwa wakisafiri kwa Treni ya Reli ya Kati wakwama Pugu.


                              Picha ikionesha treni ya reli ya kati.
Abiria waliokuwa wakisafiri kwa Treni ya Reli ya Kati kutokea jijini Dar es salaam kuelekea Morogoro,Dodoma,Tabora,Mwanza na Kigoma wamekwama na kushindwa kuendelea na safari yao hivi leo.
Inaelezwa kuwa safari hiyo tangia jana imeshishindikana hadi leo hii kwa kile kinacho elezwa kuwa baada ya Treni hiyo kufika Pugu jijini Dar es Salaam kuna ajali ambayo imetokea hivyo safari haiendelei.
Abiria waliokuwamo humo wameendelea kuitupia lawama na mamlaka husika juu ya usafiri huo ikizingatiwa wana watoto na hata kipato walicho nacho hakitoshi kwani watakitumia njiani kabla ya safari.
Abiria hao wanasema kuwa kwa hali ilivyo ya mlipuko wa kipindu pindu kwenye treni hiyo si salama kwao kwani hata vyoo vinaogofya maisha yao kwa kuwa vinaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa mda wowote hali ambayo si nzuri.
Wameomba juhudi za mapema zifanyike ili wajue hati ya safari yao kuliko kukaa njiani humo bila mafanikio yeyote yale huku wakielezwa kuna ajali imetokea inayo zuia wao kuendelea na Safari.
Taarifa Kamili.
Abiria waliokuwa wakisafiri kwa gari moshi kupitia reli ya kati wamekwama kwa saa kumi na sita katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku wakilalamikia kutelekezwa na shirika la reli Tanzania katika sehemu ambayo hakuna huduma muhimu za kijamii.
Baada ya Tambarare Halisi  kupata fununu kuhusu kukwama kwa gari moshi hilo lenye jumla ya mabehewa 12 kuelekea mikoa mbalimbali,tulifika katika eneo la pugu na kukuta baadhi ya abiria wakiwa wamechoka kutoka na njaa huku wengine wakiwa wamelala,na wengine wakipaza sauti zao kulalamikia kitendo cha kutelekezwa katika eneo hilo huku viongozi wahusika wa treni hiyo wakikimbia.
Baadhi ya wagonjwa nao wakatupa lawama kwa shirika la reli Tanzania kwa kuwatelekeza huku wakihofia maisha yao na maisha ya watoto katika eneo hilo.
Meneja uhusiano wa shirika la reli Tanzania ambaye licha ya kukiri kuwepo kwa ajali ya Treni ya mizigo kati ya Soga na Pugu, alishindwa kueleza vizuri sababu zilizowafanya viongozi walikuwa wakisafiri na treni hiyo akiwemo mkuu wa kituo cha Pugu kukimbia na kufunga ofisi.
Fuatilia Habari zetu kujua zaidi,Like Page yetu kuwa wakanza kusoma habari.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment