Image
Image

Tukio la udhalilishaji Malinzi kula sahani moja na Nyoso.

Juma Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya John Bocco msimu huu wa ligi kuu Tanzania.
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mchezaji Juma Nyoso, baada ya kufanya udhalilishaji kwa kumshika makalio mchezaji wa timu ya Azam, John Bocco ‘Adebayor’.
Kauli hiyo ya Malinzi aliitoa kupitia katika mtandao wa kijamii kwenye akaunti yake ya Twitter, ambapo alisema mchezaji huyo aliyefanya kitendo hicho, atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema ni kitendo cha ajabu ambacho hakiwezi kufumbiwa macho kitachukuliwa hatua ili kisijirudie tena.
“Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya mchezaji huyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hizi,” alisema Malinzi.
Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Nyoso alimfanyia madhambi nahodha wa timu ya Azam, John Bocco.
Tukio kama hilo liliwahi kufanywa na mchezaji huyo kwa mchezaji wa Simba, Elius Maguli na TFF ikamfungia mechi nane kwa kumfanyia kitendo hicho cha udhalilishaji.
Katika kesi hiyo Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Tukio hili liliripotiwa kutokea juzi lakini mwamuzi hakuona ila kupitia picha za mnato na kanda za video tukio hilo lilinaswa na kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya Elius Maguri msimu uliopita wakati Maguri akicheza kwenye klabu ya Simba SC.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment