Image
Image

Zaidi ya watu 80 wamekufa na wengine zaidi ya 150 wamejeruhiwa kufuatia mashambulio ya mabomu Nigeria.

Zaidi ya watu 80 wamekufa na wengine zaidi ya 150 wamejeruhiwa kufuatia mashambulio ya mabomu yaliyotokea jimbo la Borno kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Polisi na mashahidi wanasema kulikuwa na mashambulio matano ya mabomu, matatu katika
tukio la kwanza katika mji mkuu wa jimbo hilo, Maiduguri ambapo watu 54 waliuawa na
wengine 90 kujeruhiwa.
Saa mbili baadaye ilitokea milipuko mingine miwili kwenye kizuizi cha polisi na sokoni
katika mji wa Monguno kilomita 135 kutoka Maiduguri ambapo watu 27 waliuawa na wengine 62 kujeruhiwa.
Jimbo la Maiduguri ni ngome ya kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram ambacho kimeua zaidi ya watu 800 tangu Rais MOHAMMADU BUHARI ashike madaraka mwezi Mei mwaka huu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment