Image
Image

Canada kuondoa ndege zake za kijeshi kwenye mashambulio ya anga Iraq na Canada.

Canada itaondoa ndege zake za kijeshi kwenye mashambulio ya anga chini ya mseto unaongozwa na Marekani dhidi ya wapiganaji wa jihadi wa kikundi cha Islamic State huko Iraq na Canada.
Waziri Mkuu-Mteule wa Canada Bwana JUSTIN TRUDEAU amethibitisha hatua hiyo na amemuambia Rais BARACK OBAMA kuhusu uamuzi wake huo saa chache baada ya cham chake cha Liberal kushinda uchaguzi wa nchi hiyo.
Kama sehemu ya kampeni zake Bwana TRUDEAU aliahidi kurejesha nyumbani ndege za kivita za nchi hiyo zilizoko Mashariki ya Kati kufikia mwezi Machi mwakani ingawa bado hajatoa utaratibu wa kurejeshwa kwa ndege hizo.
Katika uchaguzi wa Jumatatu wiki hii Chama cha Liberal cha Bwana TRUDEAU ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Bwana PIERRE TRUDEA kilitwaa madaraka na kumaliza miaka kumi utawala wa Chama cha Conservative chini ya Bwana STEPHEN HARPER.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment